WAZIRI WA ULINZI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA FALME ZA KIARABU - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 9, 2022

WAZIRI WA ULINZI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA FALME ZA KIARABU

 WAZIRI wa Ulinzi na JKT, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) alikutana na kufanya Mazungumzo na Balozi wa Falme za Kiarabu, Balozi Khalifa Abdulrahman Al Marzouqi ofisini kwake Upanga, Jjijini Dar es Salaam.


Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha uhusiano wa muda mrefu katika Sekta ya Ulinzi baina ya Tanzania na Falme za Kiarabu hususan Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Falme za Kiarabu na Tanzania kupitia sekta ya ulinzi zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu katika maeneo mbalimbali yakiwemo mafunzo, ziara za viongozi na maeneo mengi yaliyosaidia kuendeleza mahusiano haya. Serikali imeanzisha mchakato wa kutafuta wawekezaji kutoka maeneo mbalimbali watakaokuja kuwekeza hapa nchini kupitia sektamta mbalimbali, ikiwa ni pamojana sekta ya ulinzi.

Mazungumzo yamehudhuriwa pia, na Makamishna kutoka Makao Makuu ya Wizara, Wakurugenzi na Wawakilishi kutoka Makao Makuu ya Jeshi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad