HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 9, 2022

WAZIRI WA ARDHI , NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI APIGA MARUFUKU UUZAJI VIWANJA VYA MITA 20 KWA 20 UNAOFANYWA NA MAKAMPUNI


Na Said Mwishehe,Michuzi TV

WAZIRI wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula amepiga marufu upimaji na uuzaji wa viwanja vya mita 20 kwa 20 unaofanywa na baadhi ya Kampuni zinazojihisisha na biashara ya uuzaji viwanja nchini.

Akizungumza leo Julai 8,2022 katika Banda la Wizara ya Ardhi lililopo kwenye Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Viwanja vya Sabasaba jijiji Dar es Salaam ambapo akiwa kwenye banda hilo aliikuta Kampuni inayonadi uuzaji wa viwanja vya mita 20 kwa 20.

Waziri Mabula amefafanua upimaji huo wa viwanja unaofanywa na baadhi ya kampuni hautoi kipaumbele katika mipango miji, ikiwemo kuwa na nafasi ya makazi bora yanayofikika bila usumbufu na kwamba Kampuni zinazouza Viwanja vya mita 20 kwa 20 wenyewe wanaangalia fedha tu na sio mpangilio mzuri wa makazi na matokeo yake nyumba zijajengwa na kukosekana kwa nafasi .

Amesema yeye kama msimamizi wa wizara hiyo kuna vitu anatakiwa kukemea na visijirudie na kwamba lazima tuzingatie mipango miji huku akifafanua kuna kampuni zimefanya hiyo huduma ni biashara tu lakini jambo muhimu ni kuhakikisha ardhi inapangwa, inapimwa na kumilikishwa sawasawa.

Waziri Mabula amesema kuna baadhi ya Kampuni hazitoi huduma ili watu kuwa na makazi bora ambavyo vitafikika na kuwa na nafasi ya kutosha na matokeo yake wanakata Viwanja vya 20 kwa 20, hivyo amepiga marufuku uuzaji huo wa viwanja na kampuni za namna hiyo zinatakiwa kuacha na kufuata utaratibu kwa kuzingatia ramani za mipango miji.

" Uuzaji huu wa Viwanja vya 20 kwa 20 ni hatari hata kwa wakazi wa maeneo husika kwani hata linapotokea janga kama moto ni rahisi kupoteza familia zaidi ya moja kwa kuwa itakuwa vigumu huduma kufika kwa wakati, hivyo napiga marufuku uuzaji huo wa viwanja,"amesisitiza Waziri Mabula.

Ametumia nafasi hiyo kuelezea Serikali inahitaji viwanja ambavyo wananchi wanaweza kufanya shughuli za kijamii na kudhibiti majanga yanapojitokeza.Moja ya Kampuni iliyobainika kuuza viwanja hivyo ni Kingu Survey ambayo ilikuwa kwenye banda la Wizara ya Aridhi na hivyo ameipiga marufuku kufanya biashara hiyo kwani upimaji wa viwanja haujakamilika.

"Viwanja vinavyouzwa na kampuni hii havijakamilika hivyo naitaka ofisi ya Kamishina wa Ardhi Pwani na Dar es Salaam kuifuatilia.Tumepambana na migogoro ya ardhi, hatutaki kuanzisha migogoro mengine ambayo inaweza kuzuilika.

"Kwa hiyo naagiza kampuni hiyo isitishe mara moja uuzaji wa viwanja kwakuwa havijakidhi vigezo na kamishina wa ardhi Dar es Salaam na Pwani wafuatilie uhalali wake na viwanja vilivyouzwa kama vipo kwenye kumbukumbu ya wizara,"amesisitiza.

Aidha ametoa mwito kwa wananchi wasinunue viwanja vinavyouzwa na kampuni hiyo kwani upimaji wake haujakamilika hivyo watapata matatizo.Katika hatua nyingine ameeleza sekta ya ardhi ni wezeshi na inayotegemewa na sekta nyingine kama madini, uwekezaji na biashara.

Hivyo wanaopima ardhi taratibu zianzie halmashauri anayeanzia ‘site’ asipokelewe kwani wengine wanakwenda huko kubadilisha matumizi ya mashamba.Hatuhitaji viwanja kila kona na kukosa sehemu ya kilimo."

Wakati huo huo akiwa katika banda hilo la Wizara ya Ardhi Waziri Mabula amepata nafasi ya kuzungumza na wadau waliokuwa katika banda hilo wakitoa huduma pamoja na wananchi waliofika kupata huduma za Wizara hiyo.

Pia ametoa maelekezo ya kuwepo kwa utaratibu wa kutambua kila anayehitaji huduma pindia anapoingia tu kwenye banda hilo kwa kusikilizwa anachohitaji kuhudumiwa na kisha kupelekwa eneo husika moja kwa moja.Lengo ni kupunguza muda wananchi kukaa muda mrefu kusubiri huduma.

Aidha akiwa hapo amekabidhi hati kwa baadhi ya wananchi ambao walifika kwa ajili ya kushughulika upataji hati.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk.Angelina Mabula akiwa amemshikia kipaza sauti mmoja ya wananchi waliofika banda la Wizara ya Ardhi kwa ajili ya kupata huduma ambapo mwananchi huyo amesema ameridhishwa na utolewaji wa huduma unaofanywa na maofisa wa wizara hiyo pamoja na idara zake huku akitoa ombi la kutaka muda wa kutoa huduma uongeze hata kama maonesho hayo yatakwisha katika viwanja vya Sabasaba.

Baadhi ya wananchi ambao wamepata hati zao katika banda la Wizara ya Ardhi lililopo kwenye Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendela viwanja vya Sabasaba Dar es Salaam wakiwa katika picha moja na Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk.Angelina Mabula baada ya kuwakabidhi hati zao leo.

Dk.Angelina Mabula ambaye ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akioneshwa mchoro wa ramani baada ya kutembelea banda la Wizara ya Ardhi leo.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk.Angelina Mabula akifafanua jambo baada ya kutembelea moja ya banda ambalo lipo kwenye Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa baada ya kutembelea banda la Wizara ya Ardhi katika maonesho ya Sabasaba.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk.Angeline Mabula (katikati) akimsikiliza mkazi wa Bunju B Dickson Mkoba (aliyekaa kulia)ambaye amefika kwenye banda la Wizara ya Ardhi katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa kwa ajili ya kutaka taratibu za uthamini kuhamisha miliki.Mkoba anataka kuhamishia miliki kwa mtoto wake(aliyevaa gauni nyekundu).

Matukio mbalimbali katika picha wakati Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula alipotembelea banda la wizara hilo katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.(PICHA ZOTE NA SAID MWISHEHE).No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad