HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 5, 2022

TCAA watia saini mkataba wa uwanachama wa SASO

Tanzania sasa ni mwanachama kamili wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika katika upande wa usafiri wa Anga(SASO) baada ya kutia saini mkataba wa kuridhia kuwa mwanachama.

Zoezi la utiaji saini hizo liliongozwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa ambaye amesaini mkataba huo ambao utasimamia Usafiri wa anga kwa niaba ya Tanzania. Na kuongeza kuwa kwa hatua hiyo itapelekea kufunguka kwa fursa za kujifunza miongoni mwa nchi wanachama hususani kujua wanafanya kazi vipi maana uwezo wa kusimamia Usafiri wa Anga unatofautiana baina ya nchi na nchi.

“Kwa kutumia mkataba huu tuliosaini leo hii wa SADC unaosimamia usafiri wa anga utatufanya Tanzania tuweze kujifunza kwa nchi jirani za SADC na pia nchi za SADC kujifunza kupitia Tanzania”.Alisema Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa ameongeza pia hatua hii itaifanya Tanzania kuwa tayari ki usalama wakati wote vikiwemo viwanja vya ndege vyote pamoja na Sekta ya Usafiri wa anga kwa ujumla vitakuwa salama zaidi.

Ameongeza pia kuwa anaamini katika makubaliano hayo yataifanya Tanzania kupunguza ajali zozote zile na hata zikitokea kutakuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kuweza kufanya uchunguzi wa kina na kujiridhisha tatizo lilikuwa ni nini na wapi ili baadae ilo tatizo lililosababisha ajali hiyo lisiweze kutokea tena.

Pia itawezesha viwanja vya Tanzania kuwa salama na kwa kufanya hivyo watalii wataongezeka kwa wingi sana kutokana na kuaminishwa kuwa usalama wao uko vizuri na pia hatua hii ni muendelezo wa kusimamia maagizo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuhusiana na fursa za Royal Tour.

Waziri Mbarawa amewaomba Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania( TCAA) , Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) na wadau mbalimbali wa Usafiri wa Anga kusimamia kanuni zilizopo kwenye mikataba ya namna hii ili nchi iwe salama na kuvutia watalii kuja kwa wingi na kuwaza kutumia usafiri wa anga na kukuza ajira zaidi.

Akitoa salamu za shukran mbele ya Waziri Mbarawa na hadhara hiyo iliyoshuhudia utiaji saini wa mkataba huo, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Hamza Johari alisema wito wa Waziri Mbarawa wa kutaka sasa asilimia za viwango vya kiusalama katika usafiri wa anga kupanda kutoka asilimia 67 hadi asilimia 85 litawezekana hasa baada ya TCAA kupatiwa kiasi cha Dola za kimarekani milioni 100 kwa ajili ya kujengewa uwezo ikiwa ni msaada kutoka serikali ya China.

Katika kaguzi za Shirika la kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO) zilizofanywa hapa nchini kupitia TCAA , Tanzania ilipanda kiusalama upande wa usafiri wa anga kutoka asilimia 36 hadi asilimia 67 ambayo ni zaidi ya viwango vya kidunia vinavyotambulika na ICAO ambao ni asilimia 60.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akionesha mkataba aliomaliza kusaini mkataba wa Usafiri wa Anga katika nchi ya Tanzania pamoja na Nchi nyingine za SADC uliofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Ndege wa  Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akizungumza na wadau mbalimbali wa Usafiri wa Anga wakati wa kusaini mkataba wa Usafiri wa Anga katika nchi ya Tanzania pamoja na Nchi nyingine za SADC uliofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Ndege wa  Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi , Gabriel Migire akitoa maelezo mafupi kuhusu namna serikali ilivyojipanga kusimamia mikataba yote ya usafiri wa Anga wakati wa kusaini mkataba wa Usafiri wa Anga katika nchi ya Tanzania pamoja na Nchi nyingine za SADC uliofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Ndege wa  Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Jumuhiya ya Usafiri wa Anga wa Nchi za SADC, Cleophas Samusodza akiwasilisha taarifa ya Jumuiya hiyo ilipofikia mpaka sasa wakati wa kusaini mkataba ambao utasimamia Usafiri wa Anga katika nchi ya Tanzania pamoja na Nchi nyingine za SADC ambazo zilitangulia kusaini mkataba huo
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza S.Johari akitoa neno la shukrani mara baada ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa mara baada ya kusaini mkataba wa Usafiri wa Anga katika nchi ya Tanzania pamoja na Nchi nyingine za SADC uliofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Ndege wa  Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau mbalimbali wa Usafiri wa Anga wakifuatilia mkutano wa kusaini mkataba wa Usafiri wa Anga katika nchi ya Tanzania pamoja na Nchi nyingine za SADC uliofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Ndege wa  Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad