Klabu ya kuogelea ya DSC yang’ara mashindano ya taifa - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 5, 2022

Klabu ya kuogelea ya DSC yang’ara mashindano ya taifa

 Nyota chipukizi wa klabu ya Dar es Salaam Swimming Club (DSC) wameng’ara katika mashindano ya taifa ya kuogelea baada ya kukusanya pointi nyingi na kuzidhinda klabu nyingine nane katika mashindano ya taifa.


Katika mashindano hayo yaloyofanyika kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Sekondari ya Shaaban Robert, chipukizi hao wa kuoegelea walivuna pointi 1,404.

Mashindano hayo yalishirikisha waogeleaji zaidi ya 200 kutoka klabu tisa za Tanzania Bara. Mbali ya DSC, klabu nyingine zilikuwa Bluefins, Champion Rise, FK Blue Marlins, Lake swimming club, MIS Piranhas, Mwanza Swim Club, na Taliss-IST. Mashindano yaliyodhaminiwa na Kilombero Sugar Company Limited ambao walikuwa wadhamini wakuu huku wadhamini wengine ni Burger 53, Rap & Roll, Pepsi na & L Juice.

Waogeleaji hao walishindana katika staili tano na katika umbali tofauti. Staili hizo ni butterfly, freestyle, Individual medley (IM), backstroke na breaststroke. Pia waogeleaji hao walishindana katika relay ambayo kulikuwa na ushidani mkubwa.

“Ushindani ulikuwa mkubwa katika mashindano kwani waogeleaji wote walikuwa wamejiandaa kwa lengo la kufanya vyema ikiwa pamoja na kuboresha muda wao wa kuogelea.

Nawapongeza wadhamini mbalimbali kwa kusaidia kufanikisha mashindano haya kwani rekodi mbalimbali zilivunjwa,” alisema Hadija Shebe ambeye ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mashindano hayo wa Chama Cha Kuogelea Tanzania (TSA).

Kwa mujibu wa matokeo ya mashindano hayo, waogeleaji wa klabu ya, Bluefins waliweza kukusanya pointi 1,052 na kuwa wa pili baada ya DSC huku klabu ya Taliss-IST ikikusanya pointi 1,001 na klabu kutoka Mwanza, Lake Swim Club ikikusanya pointi 834.

Klabu ya FK Blue Marlins ilivuna pointi 660 na kufuatiwa na klabu ya Mwanza (357), Champion Rise (253), MIS Piranhas (114) na klabu mpya kutoka Kigamboni, Pigec ikikusanya pointi 14.

Waogeleaji wakishindana katika mashindano ya taifa ya vijana kwenye bwawa la kuogelea la shule ya sekondari ya Shaaban Robert.
Meneja Masoko wa kampuni ya Kilombero Sugar Company Limited Olympia Fraten akikabidhi zawadi kwa muogeleaji chipukizi.
 Mwenyekiti wa Chama Cha Kuogelea cha Tanzania (TSA) Imani Alimanya (kulia) akikabidhi tuzo maalum kwa Meneja Masoko wa kampuni ya Kilombero Sugar Company Limited Olympia Fraten akikabidhi zawadi kwa muogeleaji chipukizi.
Waogeleaji wakishindana katika mashindano ya taifa ya vijana kwenye bwawa la kuogelea la shule ya sekondari ya Shaaban Robert.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad