RAIS WA ZANZIBAR DK.HUSSEIN ALI MWINYI AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI NA WAHARIRI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, July 3, 2022

RAIS WA ZANZIBAR DK.HUSSEIN ALI MWINYI AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI NA WAHARIRI

 


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akizungumza na Waandishi wa habari na Wahariri wa vyombo mbali mbali vya Serikali na Binafsi katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo,katika mazungumzo hayo amegusia masuala mbali mbali yakiwemo Miundombinu,Utalii pamoja na mengine ya kuleta maendeleo katika Taifa letu.
Wahariri na Waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali vya Serikali na Binafsi wakimsikiliza RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao leo katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo,ikiwa ni utaratibu aliouweka kuzungumzia masuala mbali mbali katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar .
Mwandishi wa ZBC Redio Abubakar Harith alipokuwa akiuliza suala kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi leo wakati wa mazungumzo na Wahariri na Waandishi wa Vyombo mbali mbali vya Habari vya Serikali na Binafsi katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Mwandishi Mwandamizi Nd,Salim Said Salim alipokuwa akimuuliza Suala Mhe.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi leo wakati wa mazungumzo na Wahariri na Waandishi wa Vyombo mbali mbali vya Habari vya Serikali na Binafsi katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Mwandishi wa Kujitegemea Siti Ali ni miongozi mwa Waandishi wa habari aliyeuliza suala kwa RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi(hayupo pichani) wakati wa mazungumzo na vyombo mbali mbali vya Habari vya Serikali na Binafsi katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo.
Katibu wa Jukwaa la Wahariri Zanzibar Nd,Salma Msangi alipokuwa akiuliza suala kwa RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo na Wahariri na Waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali vya Serikali na Binafsi katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo,ikiwa ni utaratibu wake aliouweka kuzungumzia na Waandishi kila baada ya kipindi .
Martin Kabenba Mwandishi na Mpiga picha wa kujitegemea alipokuwa akiuliza suala kwa RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo na Wahariri na Waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali vya Serikali na Binafsi katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo,ikiwa ni utaratibu wake aliouweka kuzungumzia na Waandishi kila baada ya kipindi .[Picha na Ikulu]

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad