RAIS WA SHINA INC: VIJANA TUMIENI FURSA MNAZOZIPATA NA SIO KUTEGEMEA KUAJIRIWA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, July 3, 2022

RAIS WA SHINA INC: VIJANA TUMIENI FURSA MNAZOZIPATA NA SIO KUTEGEMEA KUAJIRIWA

 Kongamano la Vijana lililoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la SHINA INC limeweza kuwafunda vijana  kuhusu kujitabua kwenye suala la elimu pamoja na ukatili na unyanyasaji wa Kijinsia. Kongamano hili limefanyika Makunduchi, Zanzibar likiwa na kauli mbiu ya Uongozi na Utawala , Wajibu wa Vijana katika kujenga Maendeleo endelevu.

Akizungumza wakati wa kufunga Kongamano hilo Rais wa Shirika la SHINA INC, Jesca Mushala amesema vijana wengi wanapata elimu kwa ajili ya kwenda kuajiliwa lakini hii ni tafsiri ambayo inakwamisha vijana wengi hapa nchini.

Amesema Elimu itakutayalisha wewe kwenda kujiajiri au kutafuta matumizi ya familia maana enzi za nikimaliza nakwenda kupata ajira hakuna kwaiyo nawategemea wanakongamano kuwa cachu wa maendeleo kwa kuanzisha ajira ili kuwainua vijana wengine kwa kuwa mshumaa unawasha mshumaa mwingine na ndio ilivyo katika maendeleo.

“Mtu akimaliza chuo anasubiri kuajiriwa kwasababu amefanya maombi ya kazi na anakaa kabisa kwa kutulia, huko ni kutotumia akili ulizozipata darasani, huko tunakotoka ana shahada mbili au tatu akajifunza vizuri kilimo na sasa yuko shambani analima na anasomesha watoto wake pamoja na kuendesha maisha ni kwasababu alikwenda darasani kusoma ule ujuzi alioupata darasani ndio anauendeleza mtaani” alisema Mushala

Pia alisisitiza vijana wengi wanasema kuwa nitajiajiri vipi wakati sina mtaji au sijawezeshwa lakini wanasahau kuwa waliwezeshwa na wazazi kwa kuwapeleka shule kwenda kuongeza ujuzi wao na kuna muda ukiona unaweza kunyanyuka na wengine basi unaweza kuungana na vijana wenzako ili mkanyayuka pamoja.

“Elimu sio tu ile unayoipata darasani bali kuna elimu unayoipata mtaani mfano kama hili kongamano linatoa elimu ya namna kujitambua na kuna vijana wengi wamefanikiwa kupitia program mbalimbali za SHINA INC na kwa sasa wamefika mbali ila inabidi vijana kujiepusha na elimu ambayo haiendani na maadili au utamaduni wa Kitanzania “ alisema Mushala

Pia amesema ili kusaidia kupunguza ukatili wa kijinsia na unyanyasaji ni mtoto wa kiume na mtoto wa kike wafundishwe kwa pamoja maadili na utamaduni wa Mtanzania kwa maana kwamba huwezi kumfundisha mtoto wa kike peke yake kwa kumueleza masuala ya ndoa, elimu pamoja na kujitambu bila kumfundisha na mtoto wa kiume kwani ili kupunguza unyanyasaji wa Kijinsia.

“Mtoto wa kiume akifundishwa vizuri ataweza kuthamini mtoto wa kike ili kusudi kesho yake asiweze kumnyanyasa mke wake.” Alisema Mushala

Rais wa Shirika la SHINA INC, Jesca Mushala akitoa elimu kwa vijana walioudhuria Kongamano Vijana lililoandaliwa na Shirika hilo wakati wa kufunga Kongamano hilo lililofanyika  Makunduchi, Zanzibar

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad