MISIKITI 100, WATU ZAIDI YA 350 TEMEKE KUCHANGIA DAMU JULAI 16 - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 7, 2022

MISIKITI 100, WATU ZAIDI YA 350 TEMEKE KUCHANGIA DAMU JULAI 16

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Temeke, Dkt. Joseph Kimaro akizungumza na waandishi wa habari katika hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Jamiiyatul Akhlaaqul Islaam (JAI), Wilaya ya Temeke, Juma Said.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Jamiiyatul Akhlaaqul Islaam (JAI), Wilaya ya Temeke, Juma Said akizungumza wakati wa kuhamasisha kuchangia damu katika hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Jamiiyatul Akhlaaqul Islaam (JAI), Wilaya ya Temeke, Juma Said.
Makamu Mwenyekiti wa Mbio za Pole(TEJA), Janeth Maseke kizungumza wakati wa kuhamasisha kuchangia damu katika hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa WIPAHS, Amina Mbaraka kizungumza wakati wa kuhamasisha kuchangia damu katika hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Afisa Afya wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Juhudi Nyambuka kizungumza wakati wa kuhamasisha kuchangia damu katika hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam.

HOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke kwa kushirikiana na Jumuiya ya Jamiiyatul Akhlaaqul Islaam (JAI) wanatarajia kuchangia damu ifikapo Julai 16,2022 jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Julai 5,2022 Katika Hospitali ya Temeke Jijini Dar es Salaam, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya hiyo Daktari Joseph Kimaro amesema kuwa waumini wa misikiti 100 ya Wilaya ya Temeke watachangia damu kwaajili ya kuokoa maisha ya watu.

Dkt. Kimaro amesema kuwa wanaamini zaidi ya 350 wataokoa maisha ya watu wengi hususani wanaojifungua na wale wanaopata ajali za barabarani wanaohitajika kuongezewa damu.

"Damu ni muhimu kwa maisha ya binadamu na asilimia kubwa ya wanaopoteza maisha wanapokuwa wanajifungua husababishwa na kupoteza damu nyingi, Kila unit moja ya damu itakayochangiwa itaweza kuokoa watu watatu, kwahiyo tukiangalia kupitia kampeni hii zaidi ya watu 1000 wataokolewa."
Amesema Dkt. Kimaro

Hata hivyo Dkt. Kimaro ametoa wito kwa watu wote watakaopata nafasi waweze kuunga mkono zoezi hilo ili kuhakikisha damu inapatikana kwa wingi, ili waweze kuokoa kinama wanaojifungua pamoja wanaopata ajali na wagonjwa wanaopungukiwa damu.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Jamiiyatul Akhlaaqul Islaam (JAI), Wilaya ya Temeke, Juma Said amesema wameamua kuandaa kwaajili ya kuokoa makundi mbalimbali ambayo yanahitaji damu.

“Damu haichagui dini, rangi, kabila wala jinsia, tunawakaribisha wote waweze kujitokeza ili kuokoa wenzetu, lakini pia hata sisi ni wagonjwa watarajiwa,”
amesema Said.

Kwa upande wa wanamichezo wa wilaya ya Temeke wakiwakilishwa na Makamu Mwenyekiti wa Mbio za Pole(TEJA), Janeth Maseke amesema kuwa wanambio za pole wilaya wapo pamoja kuhakikisha kuwa damu inapatikana ili kuokoa maisha ya watu wengi.

"Ndugu Mtanzania Utakapopata nafasi usikose kuja kuokoa maisha  watanzania wenzako." Amesema Janeth

Mwakilishi wa WIPAHS, Amina Mbaraka amesema kuwa kil mmoja ni Mgonjwa Mtarajiwa kwaiyo wapo pamoja katika Uchangiaji damu katika hospitali hiyo.

"Tunaomba kila atayepata taarifa hizi basi aje atoe Sadaka, Sadaka ambayo hajaigharamia kwa gharama yeyote na ni sadaka ambayo inaokoa maisha ya watu." Amemalizia Amina. 

Kwa Upande wa Afisa Afya wa Hospitali hiyo, Juhudi Nyambuka amewahamasisha wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwenda kuchangia damu.

"Kama tunavyojua damu haiizwi ingekuwa inanunuliwa tungeikuta stoo, damu lazima tujitolee." Amemalizia Juhudi

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad