MFS AFRICA WABADILISHANA UZOEFU NA WADAU, WAHUDUMIA WATEJA ZAIDI YA MILIONI 400 - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 15, 2022

MFS AFRICA WABADILISHANA UZOEFU NA WADAU, WAHUDUMIA WATEJA ZAIDI YA MILIONI 400

 

Mkurugenzi wa mauzo kanda ya Afrika mashariki wa Kampuni ya MFS Africa, Cynthia Ponera akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa biashara ya fedha kidijitali walipokutana jijini Dar es Salaam leo Julai 14, 2022.
Mkurugenzi wa mauzo kanda ya Afrika mashariki wa Kampuni ya MFS Africa, Cynthia Ponera akizungumza na wadau mbalimbali wa biashara ya fedha kidijitali leo Julai 14, 2022, jijini Dar es Salaam.
Meneja Mauzo M-Pesa Biashara, Kelvin Nyanda  akizungumza na wadau mbalimbali wa biashara ya fedha kidijitali leo Julai 14, 2022, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa MLN Enterprises, Lulu Nyamajeje  akizungumza na wadau mbalimbali wa biashara ya fedha kidijitali leo Julai 14, 2022, jijini Dar es Salaam.

Wadau wa Fedha Kidigitali wakibadilishana uzoefu katika hafla iliyoandaliwa na wafanyakazi wa MFS Africa jijini Dar Es Salaam leo.Matukio mbalimbali wakati wa hafla ya kubadilishana uzoefu wa kibaiashara ya fedha kidijitali jijini Dar es Salaam.
Picha na Emmanuel Massaka.

KAMPUNI ya MFS Africa imekutanisha wadau mbalimbali kwa ajili ya kubadilishana uzoefu wa kibiashara katika ufanyaji biashara kidijitali.

Mkurugenzi wa mauzo kanda ya Afrika mashariki wa Kampuni ya MFS Africa, Cynthia Ponera akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Julai 14, 2022, amesema kuwa MFS Africa ni kampuni inayowezesha miamala ya pesa kutuma na kupokea kutoka makampuni ya simu, benki na kampuni tofauti tofauti yanayojishughulisha na fedha kidijitali.

"Kampuni zote zinazojishughulisha na kutuma na kupokea pesa ndio wadau wetu wakubwa na leo hii tumekutana na wadau mbalimbali kwaajili ya kubadilishana uzoefu katika masuala ya biashara ya Miamala ya fedha kwa Kutumia teknolojia." Amesema Cynthia.

Amesema kuwa mpaka sasa wamefikia wateja zaidi ya milioni 400 wanaotumia mitandao ya simu kwa ajili ya kupokea na kutuma pesa. MFS Africa ikishirikiana na wadau zaidi ya 180 zikiwemo mabenki, kampuni za mitandao ya simu na mashirika ya kutuma na kupokea pesa kutoka nchi za nje wameweza kufikisha huduma kwenye nchi zaidi ya 34 katika Bara la Afrika. Pia MFS Africa wana ofisi tisa (9) Afrika zikiwemo nchi za Afrika Mashariki.

Kwa Upande wa Meneja Biashara wa Tigo Pesa, Ibrahim Mfalla amesema kuwa wanashirikiana na MFS Africa kutoa huduma kwa wateja wakubwa, wakati na wadogo. Amesema kuwa wanamategemeo makubwa kutoka MFS Africa ili waweze kupelekea wateja wakubwa kama wa Netflix na Facebook.

"Mategemeo mazuri Kama Tigo Pesa na MFS tutaweza kushirikiana pamoja kuhudumia watanzania na kuwarahisishia maisha yao katika Malipo Ukimfikilia Tigo pesa mfikilie na MFS Afrika kama Agrigator wa malipo kwa pamoja." Amesema Mfalla

Amesema kuwa Kampuni ya MFS Africa ni moja ya kampuni wanayofanyanayo kazi kwa karibu zaidi ili kurahisisha ufanyaji malipo kwa watanzania.

Akizungumzia namna anayowasaidia wafugaji kujiunga na MFS Africa, Mkurugenzi Mtendaji wa MLN Enterprises, Lulu Nyamajeje amesema kuwa MFS Africa ni fursa kwa wafugaji na wakulima mbalimbali nchini kuweza kufanya shughuli zao Kibiashara ili kufikia malengo ya kuuza mazao yao ndani na nje ya nchi.

"MFS Africa inakuwa Msaada Mkubwa kupitia malipo yanayofanyika, Mteja anapotaka kuuza au Kununia bidhaa nje ya nchi kwa kutuma au kupokea fedha ndani na nje ya nchi." Amesema Lulu.

Amesema kuwa mpaka sasa amewashauri wafugaji 10 kuweza kuingia kwenye ufugaji na kuweza kufuga kibiashara na kuongeza ufanisi katika kazi zao, ameongeza kuwa Kupitia MFS Africa wameweza kuona umhimu wa kuweza kuweka biashara zao vizuri na kuweza kuweka mahesabu yao pamoja na kufatilia jinsi malipo yanavyofanyika kupitia kwa wateja wao hata wanavyowalipa wafanyakazi wao.

Kwa upande wa Meneja Mauzo M-Pesa Biashara, Kelvin Nyanda amesema kuwa MFS Africa wanasaidia Makampuni yanayoshindwa kuunganishwa na M-Pesa katika utoaji huduma wake kupitia teknolojia inayotumika.

Amesema kuwa kampuni hiyo wanashirikiana nao kwa karibu katika kwenda sokoni kusaidia namna ya utoaji huduma kwa kutumia mitandao mbalimbali ya kifedha (Fedha za Kidijitali).

"Tunampango wa kuwafikia wajasiliamali wa dogo na Mama ntilie ili wateja wao waweze kulipia huduma wanayoipata kwa kutumia mitandao ya simu." Amesema Nyanda.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad