JIJI LA DAR ES SALAAM PITIENI MFUMO WA MAJI YA MVUA KUBAINI WALIOUNGANISHA KIHOLELA.- MHE.JAFO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 19, 2022

JIJI LA DAR ES SALAAM PITIENI MFUMO WA MAJI YA MVUA KUBAINI WALIOUNGANISHA KIHOLELA.- MHE.JAFO

 
WAZIRI  wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Dkt.Selemani Jafo amelitaka Jiji la Dar es salaam kupitia kitengo cha mazingira kubaini waliounganisha mfumo wa maji taka kwenye mfumo wa maji ya mvua ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

Ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akifanya ziara katika Mkoa wa Dar es salaam kujiridhisha na suala la uhifadhi, usimamizi na utunzaji wa Mazingira kwenye Soko la samaki la feri pamoja na ufukwe wa Oyster bay hususani kwenye mfumo wa maji ya mvua unaosimamiwa na DAWASA ili kujiridhisha na uunganishwaji huo kiholela.

Amesema maeneo haya ni maeneo muhimu sana yenye mkusanyiko mkubwa wa wananchi hivyo Maafisa mazingira kwa kushirikiana na NEMC wanapaswa kuongeza nguvu katika kuhakikisha misingi ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira inazingatiwa kwa kiwango kilichokusudiwa.

Ameongezaa kuwa ni dhahiri kabisa baadhi ya wananchi wameunganisha mfumo wa maji taka kwenye mfumo wa maji ya mvua unaopeleka maji baharini hali inayohatarisha maisha ya wanadamu na viumbe hai hivyo ni vema watu hao kuchukuliwa hatua za kisheria.

" Watu ni wazi kabisa wameunganisha mfumo wa maji taka kwenye mfumo wa maji ya mvua, tuko hapa katika bahari, ukiangaalia unasikia harufu mbaya, unaona mpaka kinyesi, hii haikubaliki." Mhe Dkt Selemani Jafo.

Aidha amewataka Maafisa mazingira wa Jiji la Dar es salaam kuhakikisha jukumu hilo linatekelezeka kwa haraka na wakati ili kunusuru mlipuko wa ugonjwa unaoweza kutokea na hali za wafanyabiashara pamoja na wananchi wanaokwenda kupumzika eneo la fukwe kuwa hatarini.

Katika hatua nyingine amewapongeza wafanyabiashara wa soko la feri kwa usafi wa mazingira na kujali uhai wa misitu kwa kutumia teknolojia ya gesi kukaangia samaki zao, na kuwataka Manispaa ya Kinondoni, kwa kushirikiana na DAWASA na NEMC ndani ya mwezi mmoja kukamilisha mchakato wa tathmini ya athari kwa mazingira eneo la ufukwe ili waweze kujenga vyoo.

Imeandaliwa na
Kitengo Cha Mawasiliano
NEMC

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad