HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 19, 2022

BASHUNGWA AZINDUA KIFURUSHI CHA NMB 'MWALIMU SPESHO' MKOANI KAGERA

 

 Benki ya NMB imepongezwa kwa kuwajali Walimu kupitia huduma zake mbalimbali zinazotoa masuluhisho ya kifedha kukidhi mahitaji ya kundi hilo.

Haya yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) – Mhe. Innocent Bashungwa wakati akizindua kifurushi cha NMB ‘Mwalimu Spesho - Umetufunza Tunakutunza’chenye masuluhisho mahususi kwa ajili ya kukidhi mahitaji mbalimbali ya Walimu Mkoani Kagera.

Kifurushi cha ‘Mwalimu Spesho’ kimejumuisha huduma zote zinazomuwezesha Mwalimu: Kupata Mikopo yenye riba nafuu -ikiwemo ya kujiendeleza kielimu yeye na watoto wake, mikopo ya biashara ndogo ndogo, ujenzi, vyombo vya moto kama Boda boda na Pikipiki za miguu mitatu. Kupata mkopo wa Bima yaani Insurance Premium Finance (IPF), ambayo inawezesha Walimu kulipa bima na kujikinga dhidi ya majanga mbalimbali. Lakini pia, Walimu watapata mikopo ya pembejeo na Mashine za kilimo pamoja na kupata elimu ya masuala ya kifedha.

Mhe. Bashungwa aliwaasa Walimu kutumia fursa hii kuelewa kwa kina na upana huduma mbalimbali zinazotolewa na NMB na ni jinsi gani wanaweza kunufaika nazo kwa unafuu, uharaka na ufanisi kwa wakati wote ili wazidi kuboresha hali zao za kiuchumi.

Nae, Mkuu wa Idara ya huduma za Serikali wa NMB – Bi Vicky Bushubo alisema, NMB itaendelea kuja na masuluhisho bora na nafuu kwa watanzania na uwajibikaji wake kwa jamii ukibaki kuwa katika viwango vya juu huku wakiendela kushirikiana na Serikali kuhakikisha kwa pamoja, wanasukuma mbele maendeleo ya kiuchumi ya Taifa na Watanzania kwa ujumla.

Benki ya NMB kila inapokutana na Walimu, hutumia fursa hiyo kuwahabarisha juu ya maendeleo yake pamoja na huduma mbalimbali zinazo wahusu na kupata mrejesho na mawazo yatakayo wasaidia kuendelea kuboresha huduma zao.

Mpaka sasa, NMB kupitia Mwalimu Spesho, imewafikia Walimu wa Mikoa ya Dodoma, Singida, Morogoro, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Mwanza na Kagera na bado wanaendelea kufikia Mikoa mingine.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) – Mhe. Innocent Bashungwa akioneshwa na Mkuu cha wa Idara ya huduma za Serikali wa NMB – Bi Vicky Bushubo chombo cha usafiri aina ya Boda boda ambayo inaweza kupatikana kupitia mkopo wa chombo cha usafiri ambao ni moja ya masuluhisho ya kifurushi cha Mwalimu Spesho. Wakishuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB – Bi. Aikansia Muro, Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa – Bw. Ladislaus Baraka na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe – Mhe. Julieth Nkembanyi Binyura (kulia)



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) – Mhe. Innocent Bashungwa pamoja na Mkuu wa Idara ya huduma za Serikali wa NMB – Bi Vicky Bushubo (kushoto) wakifunua pazia kama ishara ya kuzindua rasmi kifurushi cha NMB ‘Mwalimu Spesho - Umetufunza Tunakutunza’ Wilayani Karagwe Mkoani Kagera. Akishuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Karagwe – Mhe. Julieth Nkembanyi Binyura (kulia

 

Sehemu ya Walimu walioyohudhuria hafla ya uzinduzi wa NMB ‘Mwalimu Spesho - Umetufunza Tunakutunza’ katika ukumbi wa ELCT – Kayanga, Karagwe

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad