HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, July 2, 2022

BARAZA LA WAFANYABIASHARA AFRIKA MASHARIKI KUWA NA SAUTI MOJA, MWENYEKITI WA 'EABC' APONGEZWA

Mfanyabiashara Rostam Aziz akizungumza na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EABC), Angelina Ngalula wakati wa hafla ya Kumpongeza kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EABC) linalojumuisha nchi saba, katika hafla iliyofanyika jijini Dar Es Salaam Julai Mosi, 2022. MWENYEKITI wa Baraza la Taifa la Biashara la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EABC), Angelina Ngalula amesema Fursa za Kibiashara zimefunguka kwa Afrika nzima hivyo Afrika Mashariki imekuwa na Sauti Moja katika Ufanyaji biashara.


Ameyasema hayo leo Julai Mosi wakati wa kupongezwa kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo uliofanyika Juni Kigali Nchini Rwanda, amesema kuwa wafanyabiashara wa nchi za Afrika Mashariki, wanakuwa na sauti moja katika ufanyaji biashara zao ndani ya Jumuiya

Angelina amesema kuwa atahakikisha sekta ya Biashara inapata mazingira bora ya Uwekezaji ili waweze kupokea wawekezaji katika nchi za Afrika Mashariki kusimama sawa na mabara wengine.

Amesema kuwa Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki zimesaini makubaliano ya kuwa Kijiji Kimoja katika Ufanyaji biashara.

Angalina amesema kuwa Baraza hilo linajumuisha nchi saba ambazo ni Tanzania, Kenya Uganda, Rwanda, Burundi, Sudani Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo(DRC).

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara, Dkt. Godwill Wanga akizungumza wakati wa kumpongeza Mwenyekiti wa EABC amesema watahakikisha wanafanya nae kazi kwa ukaribu ili aweze kutimiza majukumu yake kikamilifu.

Amesema kuwa pamoja na biashara zinazofanyika ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki na bidhaa zinazozalishwa lazima matumizi yake yaongezeke, hivyo wanategemea kwa kipindi hiki atachosimamia Angelina kama Mfanyabishara atajua changamoto zilizopo na kuzitatua ndani ya jumuiya.

"Tunategemea atatusaidia sana kufanikisha biashara na uwekezaji ndani ya nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki, kwahiyo sisi tunafurahia kwa yeye kupata hii nafasi kwani ni mara ya kwanza kuipata nafasi hiyo kutoka Tanzania, tunategemea sana kuwa atavutia Uwekezaji katika Nchi ya Tanzania pia atavutia wafanyabiashata Tanzania." Amesema Dkt. Wanga

Amesema kuwa Kuchaguliwa kwa Mwenyekiti wa huyo Kutasaidia kukua kwa Utalii wa Tanzania na kuongezeka kwa wingi Watalii kutoka nchi za Afrika Mashariki na watu kutoka nje za nchi ya Afrika Mashariki kupitia Filamu Royal Tour ambayo Rais Samia ameisimamia kwa karibu.

Amesema kuwa katika uongozi wa Mwenyekiti Angelina atahakikisha gharama za ufanyaji biashara ndani ya Jumuiya hiyo zinapungua kwa sababu bidhaa zote ndani ya jumuiya zitakuwa zinaushindani ukilinganisha na nchin nyingine.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EABC), Angelina Ngalula akizungmza na Mfanyabiashara Rostam Aziz wakati wa hafla ya Kumpongeza kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EABC) linalojumuisha nchi saba, hafla iliyofanyika jijini Dar Es Salaam Julai Mosi, 2022.
Mfanyabiashara Rostam Aziz akizungumza na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EABC), Angelina Ngalula akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Julai Mosi wakati wa hafla ya Kumpongeza kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EABC) linalojumuisha nchi saba.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara, Dkt. Godwill Wanga akizungmza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya Kumpongeza kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EABC), Angelina Ngalula linalojumuisha nchi saba, katika hafla iliyofanyika jijini Dar Es Salaam Julai Mosi, 2022.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad