HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 29, 2022

WAANDISHI WA HABARI WATEMBELEA MITAMBO YA KUONGOZEA NDEGE KITUO CHA TCAA UWANJA WA NDEGE WA JNIA


Kaimu Meneja wa Kituo cha Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA)kituo cha JNIA, Joseph Magida akitoa maelezo kwa waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali kuhusu namna ndege za kimataifa zinavyoweza kuhudumiwa na Waongozaji wa Ndege wakati wa ziara ya Waandishi wa habari waliotembelea kwenye kituo cha kuongozea Ndege pamoja na Rada katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam
Afisa Mwongozaji Ndege Mkuu (TCAA) Godwin Kyejumba akitoa maelezo kwa waandishi wa habari kuhusu huduma ya kuongoza Ndege zinazopanda na kushuka kwenye eneo linalozunguka Viwanja vikubwa ambapo wanatoa maelezo Maalumu kwa marubani kwa njia ya redio bila kuziona na baadhi ya Viwanja uziona kwa njia ya rada wakati wa ziara ya waandishi wa habari waliotembelea kituo cha Kuongozea ndege pamoja na Rada katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mhandisi Mwandamizi wa Mitambo ya Kuongozea Ndege (TCAA), Kervin Mwakalobo akitoa  maelezo kwa waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali kuhusu kifaa cha kudhibiti na kuangazia mitambo ya kuongozea ndege iliyosimikwa katika TCAA Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Mhandisi Mwandamizi wa Mitambo ya Kuongozea Ndege(TCAA) Simon Kessy akitoa maelezo kwa waandishi wa Habari  kuhusu mitambo ya kunasa sauti wakati wa Kuongoza ndege waliotembelea kituo cha Kuongozea ndege kilichopo uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mitambo ya Kuongozea Ndege(TCAA) Mhandisi Kriston Mwala akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu kazi zinazofanywa na Rada wakati wa Ziara ya waandishi wa Habari  waliotembelea kituo cha Kuongozea ndege kilichopo uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Afisa Mwongozaji Ndege (TCAA) Godwin Monyi akitoa maelezo kwa waandishi wa habari kuhusu huduma za kuongoza Ndege zinazotua, kuondoka na kutembea kwenye Uwanja ambapo huduma hii ufanywa kwa kuziona kwa macho wakati wa ziara ya waandishi wa habari waliotembelea kituo cha Kuongozea ndege kilichopo uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaa
Muonekano wa Rada iliyopo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIC) jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad