SERIKALI YAWAPONGEZA WATOTO WA KIKE KWA KUFANYA BUNIFU ZENYE TIJA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 7, 2022

SERIKALI YAWAPONGEZA WATOTO WA KIKE KWA KUFANYA BUNIFU ZENYE TIJA

 Profesa Carolyne Nombo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu , Sayansi na Teknolojia akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi wa maadhimisho ya  sherehe ya kuwapongeza na kuwatia moyo wanafunzi  wabunifu wa kiteknolojia leo jijini Dar es Salaam. Sherehe hizo imefanyika Katika ofisi za Costech

Mkuregenzi mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na  TeknolojiaDkt. Amos Nungu  (Costech) akizungumza na waandishi habari wakati wa sherehe ya kuwapongeza na kuwatia moyo wanafunzi wabunifu wa kike kutoka shule nane za mkoani jijini Dar es Salaam.

Na Karama Kenyunko Michuzi TV
SERIKALI nchini imewapongeza na kuwaunga mkono Robotech kwa kuwawezesha wasichana kutoka shule nane za mkoani Tanga kufanya bunifu za kiteknolojia ambazo zimeweza kutoa suluhisho ya changamoto mbalimbali katika jamii.

Imesema ipo tayari kuziinua bunifu zao na kuzifanya kuwa bidhaa kamili ili ziweze kuingia sokoni kushindana na nyingine.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Carolyne Nombo amesema hayo leo Juni 6, 2022 jijjni Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya Sherehe ya kuwaongoza wasichana hao zijulikanazo kama ' Tekla Festival 2022' zinazoadhimishwa ulimwenguni kote kwa lengo la kuhamisha wanafunzi wa kike kuchukuwa masomo ya Sayansi na kuja kuweza kubuni Teknolojia za Kisayansi.

Amesema serikali itawashika mkono watoto hao kwa sababu mtazamo wake hivi sasa ni kuchochea mafanikio yatokanayo na Sayansi na Teknolojia ambayo yanatatua changamoto za kijamii.

"Hawa ni watoto wa kike Tanzania na ulimwengu nzima inajulikana kuwa mambo ya sayansi na teknoljia yanafanywa na wanaume lakini leo tumeshuhudia watoto hawa wamekuwa kielelezo cha kuwa wasichana wanaweza".

"Tunatambua mkazo ambao serikali unaweka juu ya mtoto wa kike kusoma masomo ya sayansi na haya ni matunda yake, kupitia Costech vijana hawa wameweza kutoa suluhisho la changamoto za kiteknolojia" amesema Nombo.

Amesema kuwa ameshahudia wanafunzi hao wakitengeza mifumo ya kuwasha Taa, kiti cha mgonjwa kinatembea kwa mfumo maalum na bunifu mbalimbali.

Amesema maadhimisho hayo ya Tekla Festival hupangwa na nchi za Sweden, Norway, Finland na Denmark kwa lengo la kuhamasisha wanawake katika Masuala ya teknolojia na ubunifu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Dkt. Amos Nungu amesema kuwa wajibu wa Costech ni kuwalea na kuwakuza wabunifu wote hususani wale wavumbuzi wa masuala ya kiteknolojia.

"Hapa leo tunasherehekea jitihada za vijana wetu kutoka shule nane za mkoa wa `Tanga , tuhamasishe wasichana kusoma masomo ya Sayansi sisi Costech wajibu wetu kuratibu na kulea wabunifu" amesema Nungu.

“Tunafanya kazi ya kuhamasisha na kuendeleza ubunifu ili kupata taifa lenye kujitegemea kwenye Sayansi na Teknolojia”amesema Nungu.

Amesema kuwa wanafunzi hao wametengeneza Sampuli kifani mbalimbali huku bunifu nyengine zikiwa zimekamilika kwenda kwa walaji.

Naye, Abdulwahab Issa Mkuregenzi wa usafirishaji na meneja miradi wa robotec clubs amesema taasisi hiyo imejikita kwenye kuwa saidia wasichana kwenye masuala ya Teknolojia.

Amesema kuwa wamekuwa wakiwaibua wasichana waliofanya Ubunifu wa miradi mbalimbali ya kiteknolojia.

"Kama ambavyo mmeshuhudia leo watoto wa kike walivyowasilisha project zao za ubunifu wa kisayansi wenye kutoa majibu ya changamoto za kiteknolojia"amesema Issa.

Mmoja kati ya wananfunzi hao Ismaiya Hamisi ambaye ameeleza kuwaanzisha kiti cha walemavu ambacho kasimika mfumo wa kutembe chenyewe amesema, wazo hilo alilipata baada kuona rafiki yangu mwenye ulemavu anashindwa kufika shuleni."

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad