HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 28, 2022

NBAA YATANGAZA MATOKEO YA MITIHANI YA MEI MWAKA 2022

Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) katika kikao chake cha 187 kilichofanyika chini ya Mwenyekiti wake CPA. Prof. Sylvia S. Temu imeidhinisha matokeo ya mitihani ya 95 ya Bodi kwa Watahiniwa waliofanya mitihani hiyo iliyofanyika mwezi Mei 2022 katika ngazi mbalimbali za masomo ya Bodi hiyo ya NBAA.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA, CPA. Prof. Sylvia S. Temu amesema kuwa matokeo hayo yameidhinishwa kufuatia mitihani iliyofanyika katika vituo 11 vilivyopo Tanzania Bara na Visiwani.

Amesema Jumla ya watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 6,729 kati ya hao watahiniwa 3,179 sawa na asilimia 47.2 walikuwa Wanawake na watahiniwa 3,550 sawa na asilimia 57.8 walikuwa Wanaume, kati ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mitihani watahiniwa 848 sawa na asilimia 12.6 hawakuweza kufaya mitihani hiyo kwa sababu mbalimbali hivyo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 5,881 sawa na asilimia 87.4.

CPA. Prof. Temu amesema jumla ya watahiniwa 386 wamefaulu mitihani ya Shahada ya Juu ya Uhasibu nchini yaani CPA (T). Kati ya watahiniwa hao wanawake ni 211 sawa na asilimia 54.7 na Wanaume ni 175 sawa na asilimia 45.3. Idadi hii inafanya jumla ya watahiniwa waliofaulu mitahani ya CPA kufikia 11,615 tangu mitihani hiyo ianze mwaka 1975.

Kati ya watahiniwa 386 waliofuzu kutunukiwa Cheti cha Taaluma ya juu ya Uhasibu wengi wao wametoka katika vyuo mbalimbali ambapo watahiniwa 97 sawa na asilimia 25.2 wametoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), watahiniwa 68 sawa na asilimia 17.9 wametoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), watahiniwa 48 sawa na asilimia 12.5 wametoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, watahiniwa 31 sawa na asilimia 8.1 wametoka Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) na watahiniwa 23 sawa a asilimia 6.0 wametoka Chuo cha Uhasibu Arusha.

“Kati ya watahiniwa waliofanya mitihani hiyo watahiniwa 264 ambao ni asilimia 4.5 wamefaulu mitihani katika mkao mmoja, wengine 35 sawa na asilimia 0.6 wamefaulu kwa kufaulu masomo walioyokuwa wameshindwa katika mitihani ya nyuma, wengine 911 sawa na asilimia 15.5 wamefaulu mitihani yao kwa kufaulu masomo waliyokuwa wamebakiza," amesema CPA Profesa Temu

Pia amesema watahiniwa 1,210 sawa na asilimia 20.6 wamefaulu mitihani yao na kwamba watahiniwa wengine 2,790 sawa na asilimia 47.4 wamefaulu baadhi ya masomo katika ngazi mbalimbali na watahiniwa 1,881 waliobakia sawa na asilimia 32.0 hawakufaulu mitibani yao.

Amesema katika ngazi ya awali ya Uandishi na Utunzaji wa Hesabu(ATEC I) watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 77 kati ya hao watahiniwa 03 sawa na asilimia 3.9 hawakuweza kufanya mitihani hiyo kwa sababu mbalimbali na hivyo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 74 sawa na asilimia 96.1.

Pia ameeleza kuwa kati ya watahiniwa 74 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 16 ambao ni asilimia 21.6 wamefaulu mitihani katika mkao mmoja huku mwingine 09 sawa na asilimia 12.2 wamefaulu mitihani yao kwa wamefaulu mitihani waliyokuwa wamebakiza.

Jumla watahiniwa 25 sawa na asilimia 33.8 wamefaulu mitihani yao ambapo watahiniwa 33 sawa na asilimia 44.5 wamefaulu baadhi ya masomo katika kazi hii na watahiniwa 16 waliobakia sawa na asilimia 21.6 hawakufaulu mitihani yao.

Aidha amesema katika hatua ya pili ya Cheti yaani ngazi ya uandishi na Utunzaji wa Hesabu(ATEC II) waliojisaliwa walikuwa 135 kati ya hao watahiniwa 04 sawa na asilimia 3.0 hawakuweza kufanya mitihani kutokana na sababu mbalimbali. Hivyo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 131 sawa na asilimia 97.0. Kati ya watahiniwa 131 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 25 ambao ni asilimia 19.1 wamefaulu mitihani katika mkao mmoja, mwingine 01 sawa na asilimia 0.8 wamefaulu masomo aliyokuwa ameshindwa katika mitihani ya nyuma.

Alisisitiza kuwa wengine 21 sawa na asilimia 16.0 wamefaulu mitihani yao kwa kufaulu masomo waliyokuwa wamebakiza, hivyo kwa ujumla watahiniwa 41 sawa na asilimia 35.9 wamefaulu mitihani yao. Watahiniwa 53 sawa na asilimia 40.5 wamefaulu baadhi ya masomo katika ngazi hii. Watahiniwa 31 waliobakia sawa na asilimia 23.7 hawakufaulu mitihani yao.

Amesema katika ngazi ya taaluma hatua ya awali watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 811 kati ya hao watahiniwa 111 sawa na asilimia 13.7 hawakuweza kufanya mitihani hiyo kwa sababu mbalimbali na hivyo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 700 sawa na asilimia 86.3.

Pia ameeleza kuwa kati ya watahiniwa 700 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 136 ambao ni asilimia 19.4 wamefaulu mitihani katika mkao mmoja huku mwingine 02 sawa na asilimia 0.3 wamefaulu masomo waliyokuwa wameshindwa katika mitihani ya nyuma, weninge 96 sawa na asilimia 13.7 wamefaulu masomo waliyokuwa wamebakiza waliyokuwa wamebakiza.

Jumla watahiniwa 234 sawa na asilimia 33.4 wamefaulu mitihani yao ambapo watahiniwa 353 sawa na asilimia 50.4 wamefaulu baadhi ya masomo katika kazi hii na watahiniwa 113 waliobakia sawa na asilimia 16. hawakufaulu mitihani yao.

Aidha amesema katika hatua ya kati waliojisaliwa walikuwa 3,516 kati ya hao watahiniwa 488 sawa na asilimia 13.9 hawakuweza kufanya mitihani kutokana na sababu mbalimbali. Hivyo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 3,028 sawa na asilimia 86.1, kati ya watahiniwa hao 3,028 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 30 sawa na asilimia 1.0 wamefaulu mitihani katika mkao mmoja, wengine 26 sawa na asilimia 0.9 wamefaulu masomo aliyokuwa ameshindwa katika mitihani ya nyuma.

Alisisitiza kuwa wengine 466 sawa na asilimia 14.7 wamefaulu mitihani yao kwa kufaulu masomo waliyokuwa wamebakiza, hivyo kwa ujumla watahiniwa 502 sawa na asilimia 16.6 wamefaulu mitihani yao. Watahiniwa 1,552 sawa na asilimia 51,3 wamefaulu baadhi ya masomo katika ngazi hii. Watahiniwa 974 waliobakia sawa na asilimia 32.2 hawakufaulu mitihani yao.

Katika hatua ya mwisho, waliosajiliwa walikuwa 2,190 kati ya hao watahiniwa 242 sawa na asilimia 11.1 hawakuweza kufanya mitihani hiyo kwa sababu mbalimbali. Hivyo watahiniwa waliofanya mitihani walikuwa 1,948 sawa na asilimia 88.9. Kati ya watahiniwa 1,948 waliofanya mitihani katika ngazi hii watahiniwa 57 sawa na asilimia 2.9 wamefaulu mitihani katika mkao mmoja, wengine 06 sawa na asilimia 0.3 amefaulu kwa kufaulu masomo aliyokuwa ameshindwa katika mitihani ya nyuma.

Amesema watahiniwa 339 sawa na asilimia 17.4 wamefaulu mitihani yao kwa kufaulu masomo waliyokuwa wamebakiza ambapo Watahiniwa 402 sawa na asilimia 20.6 wamefaulu mitihani yao huku watahiniwa 799 sawa na asilimia 41.0 wamefaulu baadhi ya masomo katika ngazi hii. Watahiniwa 747 waliobakia sawa na asilimia 38.3 hawakufaulu mitihani yao.

CPA Profesa Temu amesema Bodi ya Wakurugenzi wa NBAA imetoa pongezi kwa wale wote waliofuzu mitihani yao na kuwataka wale ambao hawajafuzu kutokata taama badala yake waongeze bidii zaidi katika masomo yao ili wawezo kufuzu mitihani ijayo.

Mitihani ya muhula wa kati pamoja na ile ya Astashahada ya Viwango vya Kiamataifa vya Uandaaji wa Hesabu za Taasisi za Umma (Diploma in IPSAS) itafanyika kuanzia Jumatatu tarehe 22 – Ijumaa tarehe 26 Agosti 2022.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA),  CPA. Prof. Sylvia S. Temu akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza matokeo ya mitihani ya Bodi iliyofanyika mwezi Mei 2022.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad