Na Said Mwishehe, Michuzi TV
KUMENOGA!
Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya timu ya Masala Princess Girls
kuibuka na ushindi wa mabao 14-1 dhidi ya timu ya Ukonga katika Ligi
ya wanawake ya Mkoa wa Dar es Salaam inayoratibiwa na Shirikisho la
mpira Tanzania (TFF)
Ligi hiyo imeanza rasmi leo Juni 9,2022 katika Viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam ambapo timu 10 zinashiriki ligi hiyo.
Katika mchezo wa leo kwenye
ligi hiyo timu ya Masala Princes Girls imeibuka na ushindi huo mnono
baada ya kuifunga timu ya Ukonga katika Ligi ya wanawake ya Mkoa wa Dar
es Salaam na mchezo ulikuwa wa kuvutia sana kutokana na uwezo waliokuwa
wakionesha wachezaji wa timu zote mbili.
Hata hivyo umahiri
wa wachezaji wa Masala Princes Girls uliifanya timu hiyo kuonekana moto
wa kuotea mbali wakati wote wa mchezo huku wapinzani wao wakionekana
kuzidiwa licha ya kufanya tihada za kutaka kupata matokeo mazuri.
Awali
kabla ya kuanza kwa mchezo huo wa ufunguzi wa ligi hiyo inayokwenda
sambamba na utoaji wa elimu kwa mtoto wa kike kuhusu masuala mbalimbali
Meneja Programu za Vijana CIS Ester Mpanda amesema kwenye shirika lao
kuna program ya vijana wa kike inayoitwa
Girls Talk, Girls Power.
“Mwaka
huu tuko kwenye Program ya afya na michezo na kupitia program hiyo
tumeanzisha timu ya michezo ya Watoto wa Kike inayoitwa Maisala Princes
ambayo leo imefanikiwa kucheza ligi ya wanawake ya Mkoa wa Dar es
Salaam.
“Kwa kweli kama CSI CSI mashindano haya ni kitu kikubwa
kwetu kwasababu watoto wa kike wanafanya vizuri sana na katika
mashindano haya ni mashindano makubwa, tunazo timu 10 zinazoshiriki na
zimekuwa zikifanya vizuri sana katika Mkoa wa Dar es Salaam.
“Mshindi
wa mashindano haya atakwenda kuuwakilisha mkoa wa Dar es Salaam katika
mashindano yatakayoshirikisha mikoa yote ya Tanzania yatakayofanyika
Dodoma,”amesema Mpanda huku akifafanua atakayeibuka mshindi katika
mashindano ya mikoa yote atakuwa amefuzu ligi daraja la kwanza.
“Niwashukuru wadau wa mpira wa kike, niwashukuru watu wanaotusaidia
Abec Company, tunatoa shukrani kwa CSI ambao wamekuwa na programu
mbalimbali ambazo zimejikita kutoa elimu kwa mtoto wa kike,”amesema.
Amefafanua
CSI wamekuwa na program nyingi lakini program ya Girls Talk ,Girsl
Power inaonesha kupokelewa vema na Watanzania, hivyo wataendelea
kusimamia vema mashindano hayo huku akitoa shukrani kwa Mkuregenzi
Mkazi wa CSI Stella Mpanda pamoja na Mkurugenzi na Mwakilishi wa CSI
Tausi Kagasheki anayeishi nchini Marekani.
“Tumekuwa tukifanya
kazi kama timu na kila kitu naamini kabisa ni mipango ya Mungu, tumeanza
na programu nyingi lakini hii tunaamini inakwenda kufanya vitu vikubwa
na mabadiliko makubwa hasa kwa mtoto wa kike , nishukuru sana Tanzania,
niishukuru TFF tu natamani kuona hawa watoto wanacheza mpaka nje ya
nchi,”amesema Mpanda.
No comments:
Post a Comment