HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 29, 2022

Gladness Lugenge wa Sinza ajishindia Milioni 10 za Biko

 
MKAZI wa Sinza, jijini Dar es Salaam, Gladness Gaithan Lugenge, ameingia kwenye orodha ya mamilionea baada ya kushinda fedha taslimu Sh Milioni 10, kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko inayoongoza kutoa washindi wengi, akicheza kwa kuingia live www.biko.co.tz pamoja na kuweka namba ya kampuni 505050 na kumbukumbu 2456.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Gladness alisema ni bahati kubwa kupata fedha ambazo hajawahi kuzishika tangu azaliwe, akiamini kuwa ni mwanzo mzuri katika kuyaweka sawa maisha yake kutokana na ushindi huo.

Mbali na wanaocheza kwa kupitia www.biko.co.tz, pia wanaotumia simu za kawaida nao wataendelea kucheza kama zamani kwa kutumia namba ya Kampuni 505050 na kumbukumbu namba 2456 na wote kujishindia kuanzia sh 2500 hadi milioni tano papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa zinazofanyika kila Jumapili.

Kianzio cha kucheza Biko ni sh 1000 na kuendelea ambapo Watanzania wengi wameendelea kushinda zawadi za papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa za kushinda hadi sh milioni 40, zikiwa na lengo la kuboresha maisha ya wote wanaocheza Biko.


Meneja Masoko na Mawasiliano wa Waendeshaji wa Bahati nasibu ya Biko, Goodhope Heaven kushoto akiwa na furaha wakati anamkabidhi mshindi wao Gladness Gaithan Lugenge katikati, mkazi wa Sinza, jijini Dar es Salaam, aliyeshinda Sh Milioni 10 kutoka kwenye droo kubwa iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.Kulia ni Meneja wa Uhusiano wa Bank ya CRDB, Tawi la Palm Beach Primier, jijini Dar es Salaam. Picha na Mpigapicha Wetu.


Meneja Masoko na Mawasiliano wa Waendeshaji wa Bahati nasibu ya Biko, Goodhope Heaven kushoto akiwa na furaha wakati anamkabidhi mshindi wao Gladness Gaithan Lugenge, mkazi wa Sinza, jijini Dar es Salaam, aliyeshinda Sh Milioni 10 kutoka kwenye droo kubwa iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. Picha na Mpigapicha Wetu.


Mkazi wa Sinza, jijini Dar es Salaam, Gladness Gaithan Lugenge akiwa amezishika fedha zake Sh Milioni 10 kwa bashasha kubwa wakati alipokabidhiwa katika bank ya CRDB, Tawi la Palm Beach Primier, jijini Dar es Salaam. Picha na Mpigapicha Wetu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad