Ahukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kumbaka mwanafunzi - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 3, 2022

Ahukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kumbaka mwanafunzi

 

Na Amiri Kilagalila, Njombe
MAHAKAMA ya wilaya ya Makete mkoani Njombe imemuhukumu Faison Sanga (19) mkazi wa Makwaranga kata ya Ipelele kutumikia kifungo cha miaka 30 gerezani kwa kosa la ubakaji

Mnamo tarehe 12.2 2022 Bwana Faison sanga anatajwa kufanya kitendo hicho cha ubakaji kwa mwanafunzi wa shule ya msingi ( 15 ) .

Kosa hilo la ubakaji ni kinyume na kifungu cha 130 ( 1 ) ( 2 ) e na 131 ( 1 ) ya kanuni ya adhabu sura ya 16 Marejeo 2019 .

Aidha Bwana Sanga ameiomba mahakama kuweza kumpunguzia adhabu kwa kuwa ana familia inayomtegemea.

Kwa upande wa mashtaka uliiomba Mahakama kuweza kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine ambao wamekuwa wakikatisha masomo ya watoto wa kike.

Kwa upande wa mashtaka mashahidi wa kesi hiyo walikuwa wanne ambao ni muhanga mwenyewe,baba wa mtoto,Daktari kutoka hospitali ya wilaya ya Makete pamoja na G3615 Dictective Coplo Benedicto .

Hukumu hiyo imetolewa hapo jana na hakimu mkazi mfawidhi wilaya ya Makete Mh.Ivan Msaki pamoja na Inspecta wa jeshi la polisi Benstard Mwoshe Wilaya ya Makete.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad