HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 10, 2022

UONGOZI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM WATEMBELEA SUPERDOLL

Mwenyekiti wa Makampuni ya Supedoll, Seif Seif (wa tatu kulia) akizungumza jambo na Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es salaam, Prof. William Anangisye (wa pili kulia) aliyetembelea Kampuni ya Superdoll, iliyopo Barabara ya Pugu, jijini Dar es salaam, mwishoni mwa wiki. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam na ujumbe wake walifanya ziara ya kutembelea kiwanda hicho kwa lengo la kuona uwekezaji wa kampuni hiyo pamoja na kuangalia namna nzuri ya kushirikiana.  Kulia ni Meneja Mkuu wa Superdoll, Ibrahim Juma.
Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es salaam, Prof. William Anangisye akifafanua jambo kwa Uongozi wa Kampuni ya Superdoll, katika kikao chao kilichofanyika kwenye ofisi za kampuni hiyo, iliyopo Barabara ya Pugu, jijini Dar es salaam, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Prof. Benadetha Kilian.
Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es salaam, Prof. William Anangisye akimueleza jambo Mwenyekiti wa Makampuni ya Supedoll, Seif Seif wakati wakiwa kwenye ziara ya kutembelea sehemu ya vitengo vya Kampuni hiyo, iliyopo Barabara ya Pugu, jijini Dar es salaam, mwishoni mwa wiki.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad