HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 20, 2022

SHAMRASHAMRA ZAZIDI KUPAMBA MOTO KUELEKEA KUWASILI ZIARA YA KOMBE LA DUNIA LA FIFA NA COCA-COLA MEI 31, 2022, NCHINI TANZANIA

 
Tanzania ni miongoni mwa nchi 54 duniani na tisa barani Afrika kupata fursa ya kuwa mwenyeji wa ziara ya kombe hilo baada ya miaka 8. Ziara hiyo ni sehemu ya utamaduni wa Coca-Cola kusherehekea na kushiriki furaha ya kila mashindano ya Kombe la Dunia na mashabiki pamoja na watumiaji wake kupitia ushirikiano wake wa muda mrefu na FIFA.

Kombe la Dunia linatarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere Mei 31 majira ya saa 11 asubuhi. Litakaribishwa na viongozi mbalimbali wa serikali na michezo akiwemo Waziri wa Michezo, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, na uongozi wa Coca-Cola Tanzania.

Baada ya kutua, viongozi wachache wa serikali na wageni waliochaguliwa wataruhusiwa kutazama kwanza kabla ya msafara huo kuelekea Ikulu ambapo Mheshimiwa Rais, Samia Suluhu Hassan atalipokea rasmi na kulishika. Kwa mujibu wa sheria za FIFA, ni Mkuu wa nchi pekee ndiye anayeruhusiwa kulishika kombe hilo, wengine watastahili kulitazama na kupiga nalo picha. Mara ya mwisho kombe hilo kuzuru Tanzania ilikuwa mwaka 2013 ambapo liliandaliwa na aliyekuwa Rais wa nne wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Tofauti na miaka ya nyuma, wateja wa Coca-Cola Tanzania na mashabiki wa soka watakaopata fursa ya kuliona kombe hilo kwa ukaribu zaidi na kupiga nalo picha, tukio ambalo litafanyika katika Uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa, Juni 1, 2022. Kwa sasa kuna matukio kadhaa ya shamrashamra yakiendelea mikoani ambapo Watanzania wanaweza kujishindia tiketi maalum na zawadi kemkem.

Michuano ya Kombe la Dunia la FIFA 2022 itafanyika nchini Qatar kuanzia Novemba 21 hadi Desemba 18. Afrika itawakilishwa na nchi tano katika mashindano hayo ambazo ni Senegal, Ghana, Morocco, Tunisia, na Cameroon.

HATA WANAWAKE TUNAWEZA……baadhi ya wateja na mashabiki wa jijini Arusha waliojitokeza wakati wa matukio ya shamrashamra za kuelekea kuwasili kwa Ziara ya Kombe Halisi la Dunia la FIFA nchini Tanzania kwa kushirikiana na Coca-Cola. Kombe hilo linatarajiwa kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Mei 31, 2022 ambapo litapelekwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan ambapo atalipokea na kulishika kwa niaba ya Watanzania wote. Wateja na mashabiki wa soka nchini watapata fursa ya kuliona kwa karibu na kupiga nalo picha Juni 1, 2022 Katika Uwanja wa Taifa wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam. NJUMU SIO KIKWAZO, DANADANA TU HAPA…… baadhi ya wateja na mashabiki wa jijini Arusha waliojitokeza wakati wa matukio ya shamrashamra za kuelekea kuwasili kwa Ziara ya Kombe Halisi la Dunia la FIFA nchini Tanzania kwa kushirikiana na Coca-Cola. Kombe hilo linatarajiwa kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Mei 31, 2022 ambapo litapelekwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan ambapo atalipokea na kulishika kwa niaba ya Watanzania wote. Wateja na mashabiki wa soka nchini watapata fursa ya kuliona kwa karibu na kupiga nalo picha Juni 1, 2022 Katika Uwanja wa Taifa wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.
NI MSISIMKO, VIFIJO NA NDEREMO……. baadhi ya wateja na mashabiki wa jijini Arusha waliojitokeza wakati wa matukio ya shamrashamra za kuelekea kuwasili kwa Ziara ya Kombe Halisi la Dunia la FIFA nchini Tanzania kwa kushirikiana na Coca-Cola. Kombe hilo linatarajiwa kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Mei 31, 2022 ambapo litapelekwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan ambapo atalipokea na kulishika kwa niaba ya Watanzania wote. Wateja na mashabiki wa soka nchini watapata fursa ya kuliona kwa karibu na kupiga nalo picha Juni 1, 2022 Katika Uwanja wa Taifa wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad