HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 21, 2022

SERIKALI ITASHIRIKIANA NA KILA MDAU MWENYE NIA NJEMA YA KUWANUFAISHA WAKULIMA

 

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe .Anthony Mavunde akizungumza wakati wa uzinduzi wa programu ya Afrika Connection jijini Dodoma.

Picha ya Pamoja.

Na Janeth Raphael - Dodoma
SERIKALI imeahidi kuendelea kushirikiana na sekta binafsi kuinua sekta ya Kilimo na kuboresha maisha ya wananchi wanaojishughulisha na Kilimo.

Akizungumza jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa programu ya Afrika Connection, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe .Anthony Mavunde amesema ili kufikia malengo ya kukuza sekta ya Kilimo kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030 serikali itashirikiana na kila mdau mwenye nia njema ya kuwanufaisha wakulima na Taifa kwa ujumla.

Mhe. Mavunde ameongeza kuwa serikali haitashirikiana na taasisi ambayo itaonesha dalili za kudhulumu au kuwanyonya wakulima.

"Kabla ya kuja kushirikiana nanyi kwenye uzinduzi wa programu hii nilitumia muda wangu kujiridhisha kama hili suala lina maslahi kwa wakulima". Amesema Mhe. Mavunde.

Mhe. amezishauri kampuni zinazoshirikiana kwenye programu hiyo ambayo inalenga kuwawezesha wakulima wa mpunga kuanzia uzalishaji hadi kutafuta masoko, kuongeza wigo wakuwafikia wakulima wa mazao mengine ili kukuza sekta ya Kilimo na kuinua uchumi wa wakulima.

Mhe. Mavunde amewataka wadau wote wa Kilimo kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwani ni Kiongozi anayeingalia sekta ya Kilimo kama njia sahihi ya kutatua changamoto za kiuchumi hasa ukose wa ajira kwa Watanzania hususan Vijana.

Amesema serikali imejidhatiti kuwekeza kwenye utafiti na uzalishaji wa mbengu ili nchi ijitosheleze kwa mbegu na ziada iuzwe nje ya nchi.

Mhe. Mavunde ambainisha kuwa hatua ya Rais Samia Suluhu Hassan kuongeza bajeti ya umwagiliaji kutoka shilingi Bilioni 51 Mwaka 2021/2022 hadi Bilioni 361 Mwaka 2022/2023 ni kuelekea kwenye kuipa nchi uwezo wa kuendesha shughuli za kilimo bila ya kutegemea mvua.

Program ya Aficaconnect inalenga kuwasaidia wakulima wa mpunga kueza kupata mikopo pamoja na huduma za miongozo ya uzalishi wa mpunga na hatimaye kuwaunganisha na masoko.

Awali akizungumza kabla ya uzinduzi huo, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu Bora za Kilimo Tanzania ASA, Dkt. Sophia Kashenge amesema wakulima wanahitaji mbegu bora ili waweze kumudu ushindani kwenye biashara ya mazao na ASA imejipanga kuhakikisha wanazalisha mbegu bora kwa s wakulima.

Programu hiyo itaendeshwa kwa ushirikiano kati ya Wakala wa Mbegu Bora za Kilimo (ASA), Benki ya Equity,Kampuni ya waagizaji uzalishaji na usambazaji wa mbolea Yara, Wilmar na Colteza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad