HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 20, 2022

MUHAS kitengo cha Afya ya kinywa na Meno wapokea msaada wa mashine ya kisasa

 

Balozi was Uturuki nchini Tanzania Dkt. Mehmet Gulluoglu, (katikati) akipokea zawadi kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Chuo Muhas, Profesa Appolinary Kamuhabwa,  wa kwanza kulia ni Mkuu wa shule ya kinywa na Meno Muhimbili, Dkt. Matilda Mtaya.
Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Dkt, Mehmet Gulluoglu akizindua mashine leo Mei 20, 2022 Jijini  Dar es Salaam kabla ya kukabidhi mashine hiyo itakayosaidia matibabu ya kinywa na Meno katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili (MUHAS) yenye thamani ya zaidi ya sh. Milioni 200.
Wajumbe kutoka Shirika la Ushirikiano na Uratibu la Uturuki (TIKA) wakifuatilia hotuba ya Kaimu Mkuu wa Chuo Muhas, Profesa Appolinary Kamuhabwa,  wakati wa hafla ya kukabidhiwa mashine ya kusaidia matibabu ya Kinywa na Meno leo Meo 20,2022 jijini Dar es Salaam
Mkuu wa shule ya Afya ya Kinywa na Meno Muhimbili,  Dkt,  maltrida Mtaya akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa Mashine itakayosaidia, matibabu na vipimo vya kinywa na Meno leo Mei 20, 2022 jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wanafunzi na wakufunzi wa Afya ya Kinywa na Meno na wakifuatilia hotuba ya Kaimu Mkuu wa Chuo Muhas, Profesa Appolinary Kamuhabwa,  wakati wa hafla ya kukabidhiwa mashine ya kusaidia matibabu ya Kinywa na Meno leo Meo 20,2022 jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Dkt, Mehmet Gulluoglu akizungumza na wauguzi Pamoja na uongozi wa Chuo, leo Mei 20, 2022 Jijini  Dar es Salaam baada ya kukabidhi mashine itakayosaidia matibabu ya kinywa na Meno katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili (MUHAS) yenye thamani ya zaidi ya sh. Milioni 200.
Picha ya Pamoja.

CHUO Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili (MUHAS) kitengo cha Afya ya kinywa na Meno kimepokea msaada wa mashine ya kisasa ya Cone-beam Computerized Tomographic

(CBCT) kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa ya kinywa na meno chenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 200

Mashine iliyotolewa na serikali ya Uturuki, ni ya kwanza kupatikana katika hospitali za serikali hapa nchini na imeelezwa kuwa ni suluhisho kwa wagonjwa wanaosubiri muda mrefu kwa ajili ya uchunguzi wa kinywa na meno kwa kuongeza kasi ya kuwapima wagonjwa wengi zaidi na kuondoa msongamano wa kusubiri vipimo kwa muda mrefu.

Akizungumza mara baada ya kupokea mashine hiyo, leo Mei 20,2021 jijini Dar es Salaam, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha (MUHAS), Profesa Appolinary Kamuhabwa amesema mashine hiyo ina uwezoo wa kupima na kutambua Kwa haraka magonjwa ya kinywa na meno

Profesa Kamuhabwa amesema uhusiano mzuri uliopo kati Tanzanaia na Uturuki ndio umewezesha kupatikana kwa mashine hiyo ya Kisasa ambayo inaenda kuwa msaada kubwa hospitalini hapo na kwa wanafunzi wa shule ya kinywa na meno.

Naye Balozi wa wa Uturuki nchini Tanzania Dkt. Mehmet Gulluoglu ameahidi kuendeleza ushirikiano mwema katika kuimarisha sekta ya afya nchini huku mtaalamu wa magonjwa ya kinywa na meno wa hospitali hiyo Dkt.Karpal Sigh akiweka bayana ufanyaji kazi wa mashine hiyo.

Kwa upande wake, Mkuu shule hiyo nchini, Dkt. Matilda Mtaya amesema watu wengi wanasumbuliwa na matatizo ya fizi, meno kutoboka na harufu mbaya kinywani

Amesema, kupatikana kwa mashine hiyo kunaashiria mwanzo wa kiwango kingine cha uboreshaji wa mafunzo na umakini wa matibabu katika shule hiyo katika kujifunza na kufanya tafiti mbalimbali za magonjwa ya kinywa na meno.

Amesema, Chuo hicho tangu kuanzishwa kwake mwaka 1979 kimekuwa kikijitahidi kutoa huduma bora kwa wananchi wote na mafunzo ya kliniki kwa wanafunzi wa meno yanayopatikana

"Tangu kuanzishwa kwa Chuo hiki mwaka 1979, tumekuwa tukijitahidi sana kutoa huduma bora kwa watu wote. Vile vile, tumekuwa tukijitahidi kutoa mafunzo bora zaidi ya kliniki kwa wanafunzi wa meno ndani ya njia zinazopatikana"

Amesema, mwaka 2014 chuo kilianzisha mfumo wao kidijitali wa taarifa za wagonjwa ambao ulijumuisha uwekaji wa mifumo ya picha yaani periapical x-rays and Orthopantomography (OPG) ambazo hata hivyo zilikuwa zikitoa picha za pande mbili tu ambazo hazitoshi kufanya uchunguzi sahihi na upangaji wa matibabu kwa ajili ya taratibu za kisasa za meno kama vile matibabu ya Endodontic, Implantology, na hata baadhi ya matukio ya kiwewe na matatizo ya viungo vya temporomandibular.

"Mashine hii inaifanya Shule yetu kuvuka hatua nyingine muhimu katika uwanja wa uchunguzi wa matibabu kwa Madaktari, Wagonjwa na wanafunzi wa kliniki ambao watafaidika sana kwa kutumia mashine hii.

Hii sio mara ya kwanza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kunufaika na msaada wa vifaa tiba zinazotolewa na wahisani mbalimbali kuwezesha ikiwa ni sehemu ya kuunga juhudi za serikali kutoa huduma bora kwa Watanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad