HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 20, 2022

CSI WAJA NA MASALA PRINCESS GIRLS ITAKAYOMUWEZESHA MSICHANA KUTIMIZA NDOTO ZAKE

 

 


Na Said Mwishehe, Michuzi Tv
SHIRIKA la Childbirth Survival International (CSI) ambalo limejikita kwenye kampeni ya kuzuia vifo vya mama mjazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano limeamua kuja na program maalum ya michezo wa mpira kwa watoto wa kike iliyopewa jina la Masala Princess Girls.

Akizungumza katika mahoajiano maalum Meneja Programu Vijana kutoka CSI Ester Mpanda amesema pamoja na kujikita katika kupunguza vifo vya watoto lakini wamekuwa wakijihusisha na program za watoto wa kike.

“Katika CSI tuna program tofauti tofauti lakini main program ambayo tunayo ni Girls Talk, Girls Power ambayo inamhumsisha mtoto wa kike katika makuaji na maendeleo yake ya kiafya , kimwili na kiakili, CSI ilipoanzisha program hii ilikutana na wadau mbalimbali na mmoja wa wadau wa muda mrefu ni JK Youth Pack ambaye amekuwa mdhamini.
“Tumekuwa tukiita watoto kutoka shule mbalimbali zilizopo jijini Dar es Salaam na kukutana hapa uwanjani kwasababu tunajua ni sehemu ambayo watoto wanapenda kuja kushiriki michezo, kwa hiyo tunakutana nao na kuzungumza masuala yanayohusu makuaji.

“Katika program hiyo mwaka huu tukapata wazo tofauti kidogo hivyo tukaamua kuanzisha timu ya watoto wa kike ya mpira inayoitwa Masala Princess. Katika timu ya Masala Princes mimi ni Mtendaji Mkuu wa timu hiyo yaani CEO na ndio mwanzilishi lakini tunao wakurugenzi, tunao makocha na timu inafanya vizuri,”amesema Mpanda.

Ameongeza kutokana na mahusiano mazuri kati yao na JK Pack ambao ni wadhamini wao wamepewa nafasi ya kufanya mazoezi.Pia wanaye mdhamini mwingine Abec Company inayojihusisha na vifaa vya ujenzi lakini kwenye Masala Princess wamekuwa wakitoa vifaa vya michezo.

Akifafanua zaidi kuhusu Masala Princess, Mpanda anasema katika miaka minne ijayo wanatarajia kuwa na timu za watoto wa kike kuanzia umri wa miaka 14 hadi miaka 17.
“Nia yetu ni kukuza michezo kwa watoto wa kike, kuimarisha afya na akili, mtoto akicheza na akili inachangamka.Michezo pia inamuondoa mtoto wa kike kwenye mambo yanayoweza kuua ndoto zao kama kujihusisha na dawa za kulevya na mimba za utotoni,”amesema.

Ameongeza kwa hiyo michezo kwao imekuwa na
namba moja na katika programu ambazo CSI wamefanya Massala Princess ni miongoni mwa program bora kabisa.“Wakati tunaanzisha program hii walikuja baadhi ya wasichana wakiwa na changamoto nyingi hata kwa muonekano.

“Baada kuanza kujihusisha na program hii ya Masala Princess wameanza kubadilika. Niwaombe wadau wa mpira hasa wanaojihusisha na watoto wa kike wasaidie kwani watoto wa kike wanapita kwenye changamoto nyingi ambazo nyingine ni za kimaumbile.

“ Masala Princess bado ndogo kwa hiyo tunahitaji wadau wengi ili kutimiza ndoto za wasichana,” amesema na kuongeza watoto wa kike walioko Masala Princess wanapaswa kupewa tumaini na kuaminishwa kuna maisha mbele yao na kokote watakakokwenda basi waende kwa ajili ya kuiwakilisha nchi na wala sio wao au familia zao

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad