HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 26, 2022

MSD WATEMBELEWA NA WABUNGE WA BUNGE LA ZAMBIA, WAONDOKA NA KIWANDA CHA BARAKOA

Mmoja ya Wabunge wa Bunge la Zambia akiangalia mitambo ya kiwanda cha barakoa kilichopo katika Bohari ya Dawa jijini Dar es Salaam leo, Mei 26,2022.
Wabunge wa bunge la Zambia na wajumbe wa kamati huduma za jamii na Afya ya bunge la Zambia wakitembelea Bohari ya Dawa (MSD) leo Mei 26,2022jijini Dar es Salaam.

BOHARI ya Dawa (MSD) leo Mei 26,2022 wametembelewa na wabunge wa Bunge la Zambia kwaajili ya kuangalia namna Bohari hiyo ya dawa inavyofanya kazi ukilinganisha na bohari ya Dawa (ZAMBRA) nchini Zambia.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja Mawasiliano na Uhusiano kutoka Bohari ya Dawa (MSD), Etty Kusiluka amesema kuwa ugeni huo wa wabunge wa Zambia ni wajumbe wa kamati huduma za jamii na Afya ya bunge la Zambia.

"Wametaka kujua Bohari ya dawa imeanza uzalishaji wa bidhaa za afya kutokana na maboresho ya mabadiliko ya sheria ambapo sheria imeruhusu MSD kuweza kuzalisha bidhaa za afya na tumeweza kuzalisha tangu mwaka jana." Amesema Etty

Amesema ujumbe huo kutoka Zambia Umeweza kutembelea viwanda viwili, ambapo wametembelea kiwanda cha KPI ambacho kinazalisha dawa 10 tofauti na kiwanda cha kuzalisha barakoa.

"Dawa hizi 10 saba ni 'antibiotics', Moja dawa ya Fangasi na mbili ni dawa za kutuliza maumivu." Ameeleza Etty

Amesema wametembelea MSD kwasababu na Zambia wamebadilisha sheria na kuwawezesha kuanza Uzalishaji wa bidhaa za afya ukitofautisha na ilivyokuwa mwanzo walikuwa wananunua, wanatunza na kusambaza dawa na vifaa tiba tu.

Kwa Upande wa Mwakilishi wa wabunge wa Zambia kutoka kamati ya huduma za jamii na Afya amesema kuwa watazungumza na ZAMBRA ili wafanyakazi MSD waende kutembelea viwanda vya Zambia kwaajili ya kubadilishana uzoefu katika hatua za utekelezaji wa masuala ya uzalishaji wa bidhaa za afya.

Hata hivyo wamepongeza kwa hatua zilizopigwa na MSD kuwa na Viwanda 41 vya uzalishaji wa dawa na vifaa tiba.

Amesema kuwa kitu cha kwanza kuchukua ni kwenda kushauri serikali yao kuanza kuzalisha barakoa kama MSD inavyozalisha ili kuepukana na gharama za kununua barakoa kutoka nje ya nchi.

Amesema kuwa Tanzania imechukua mfumo wa (Public, Private join ventures) PP na watajifunza kutokana na mfumo unaotumiwa na Watanzania katika viwanda vya uzalishaji dawa na vifaa tiba kuwa serikali inakuwa na uwekezaji katika viwanda hivyo.

Mitambo ya Kiwanda cha Barakoa kilichopo Bohari ya Dawa (MSD)


Wabunge wa Bunge la Zambia wakiwa katik kiwanda cha kuzalisha Barakoa kilichopo MSD jijini Dar es Salaam.






Wabunge wa Bunge la Zambia wakipata maelezo katika eneo la kuhifadhi dawa katika bohari ya dawa
Wabunge wa bunge la Zambia wakiingia katika eneo la kuhifadhia dawa dawa.







Meneja Mawasiliano na Uhusiano kutoka Bohari ya Dawa (MSD), Etty Kusiluka akizungumza wakati wabunge wa bunge wa Zambia walipotembelea Bohari ya Dawa leo jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Mavere Tukai akizungumza wakati waunge wa Bunge la Zambia walipotembelea Bohari ya Dawa leo jijini Dar es Salaam.






No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad