HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 26, 2022

Watanzania waaswa kutumia bima ya kiislamu ya Takaful

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mayzuh, Mohamed Hemed akiwasilisha mada wakati wa Mafunzo mafupi ya bima ya kiislamu ya Takaful yaliyofanyika leo Mei 26,2022 Jijini Dar es Salaam.
Meneja Kanda ya Pwani wa Shirika la Bima Zanzibar Bi, Majda Issa Ahmed (kushoto) akifuatilia Mafunzo mafupi ya bima ya kiislamu ya Takaful yaliyofanyika leo Mei 26,2022 Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wadau wa Bima nchini wakifuatilia mafunzo mafupi ya Bima ya kiislamu ya Takaful yaliyofanyika leo Mei 26,2022 Jijini Dar es Salaam.

WATUMIAJI wa Huduma za Bima nchini wameshauriwa kutumia Bima ya Dini ya kiislamu ya Takaful kutokana na kuwa na faida nyingi ikiwemo ya kugawana faida kati ya kampuni husika na mtumiaji pale inapokwisha muda wake.

Ushauri huo umetolewa mapema leo jijini Dar es salaam, na meneja kanda ya pwani wa shirika la bima Zanzibar, Majda Issa Ahmed wakati wa Mafunzo mafupi ya bima ya kiislamu ya Takaful.

Ahmed amesema kuwa uwepo wa bima hiyo umesaidia kuwatoa hofu watu wenye imani ya kuwa bima ni kamali kwani ukitumia Takaful na muda ukaisha pasipo kuitumia kampuni hiyo itagawana faida na mteja kulingana na ilivyopatikana.

Amesema kuwa Bima hiyo itaongozwa kwa misingi ya Dini ya kiislamu na kufuata sheria za mamlaka ya uzima wa bima nchini (TIRA), hivyo kusaidia watumiaji kunufaika.

Aidha amesema kuwa bima hiyo ni ngeni hapa nchini hivyo kutoa mafunzo hayo kwa mawakala na madalali ili kuweza kusaidia wao kuwafikia watu wengi zaidi na elimu kusambaa kwa uharaka.

Ameongeza kuwa kwa sasa wako tayari kuingia sokoni isipokuwa kuna maboresho machache yanafanywa na TIRA lakini mpka kufikia mwezi Juni Wanatarajia kuanza kazi.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Mayzuh, Mohamed Hemed amesema kuwa mfumo wa bima ya Takaful ni ambao wanaotumia wanakata kwa msingi wa kuchangia kwenye kukidhi Majanga baina yao halafu kampuni inakuwa ni msimamizi wa ule mfuko unaotokana na kuchangia ikiwa lengo ni kusaidiana kwa kuleana.

Nao baadhi ya washiriki wa Mafunzo hayo ya bima ya Takaful ikiwemo mawakala na Madalali wamesema kuwa ujio wa Bima hiyo utawarahisishia watu wenye msimamo mkali wa dini kuweza kutumia Huduma hiyo kwani suala la wasiwasi wa uwepo wa kamali haupo kutokana na wahusika wote kunufaika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad