Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Manyara
CHAMA
Cha Mapinduzi( CCM) kimewaelekeza watendaji wenye dhamana wa serikali
kushuka ngazi za chini na kuzisikiliza changamoto na kero zinazowakabili
wananchi na kuzipatia utatuzi huku akikitoa rai kwa viongozi
kutekeleza maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan bila kuathiri shughuli
zinazofanywa na wananchi katika kujitafutia kipato.
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Shaka Hamdu Shaka ameleeza hayo wakati
akizungumza na wajasiriamali wadogo na wakati wakiwemo Machinga, Mama
Lishe na waendesha bodaboda eneo la Stendi ndogo ya Mabasi Babati Mjini.
Shaka
baada ya kufika kwenye stendi hiyo alipata nafasi ya kusikiliza
wananchi akiwa kwenye kijiwe cha kuuza Kahawa ambapo miongoni mwa
malalamiko aliyopewa ni uwepo wa manyanyaso yanayofanywa na baadhi ya
mgambo kwa wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama Machinga.
“Si
vema kwa watendaji wenye dhamana wa serikali kuu na serikali za mitaa
kujiweka mbali bila kufuatilia matatizo yanayowakera wananchi kwa kupata
bughudha mbalimbali ikiwemo mgambo wa halmashauri za wilaya, manispaa
na miji midogo na majiji wanaowanyanyasa wajasirimali wajapokuwa katika
shughuli zao za uzalishaji mali.
“ Lengo la Rais Samia Suluhu
Hassan kuagiza wafanyabiashara ndogo ndogo wapangwe Chama Cha Mapinduzi
tunaliunga mkono kwa asilimia 100, tunataka kuona wafanyabiashara
wanakaa katika maeneo salama na kufanya biashara zao bila kusumbuliwa.
“Tunashauri
wenzetu wa Serikali kutekeleza maelekezo ya Rais kwa kuhakikisha
maeneo ya kufanya biashara yanakuwa rafiki , tunataka kuona
wafanyabishara wanaongezeka mitaji yao , hatutaki kuona wafanyabiashara
wanafilisika kibiashara, tunataka wakuze biashara zao kwa kuhakikisha
wanawekewa mazingira rafiki,” amesema Shaka.
kila siku,” amesema Shaka.
Katibu
huyo wa Itikadi na Uenezi Taifa akiwa kwenye kijiwe hicho cha kahawa
amepata nafasi ya kusikiliza kero za wananchi na kupitia hekima,busara
alizonazo ametoa utatuzi wa changamoto hizo hali iliyofanya kuibua
shangwe kwa wananchi wanyonge hasa wanaojihusisha na biashara
ndogondogo.
Shaka amesema kuwa kazi ya CCM ni kuisikiliza
wananchi na wakishasikiliza wanatafuta ufumbuzi kwa kuishauri Serikali
namna nzuri ya kushughulikia matatizo ya wananchi, huku akieleza pamoja
na uwepo wa sheria na taratibu bado kuna kila sababu ya viongozi kutumia
sahihi kutafuta suluhu bila kuharibu shughuli za watu.
Awali
mmoja ya wajasiriamali mdogo anayejihusisha na uuzaji wa matunda na
mbogamba akizungumza kwa niaba ya wajasiriamali wengine wadogo hasa
wanawake kueleza kwamba katika zoezi la kupanga wamachinga katika maeneo
ya Babati yamewaweka katika mazingira magumu kibiashara, hivyo wanaomba
waruhusiwe kufanya biashara nyakati za usiku.
Amesema kuwa
walikopelekwa sio mazingira rafiki kwa kufanyabiashara kwani ni eneo
ambalo wamewekwa pamoja na wafanyabishara ambao ni wakulima wanaokuja
kuuza mazao, hivyo wao kushindwa kuuza ukizingatia wengi wao wamekopa na
wanaendesha maisha yao kwa kutumia biashara hizo ambazo nyingi ni za
kuuoza haraka iwapo watashindwa kuuza kwa wakati.
Aidha
wafanyabiashara wengine kwenye stendi hiyo ya zamani wametoa ombi kwa
Shaka kuwaombea kwa viongozi wa Serikali kama itawezekana daladala
zirudishwe eneo hilo kwani biashara zao zimekuwa ngumu kidogo huku
wakizungumzia umuhimu wa kuboreshwa eneo hilo.
No comments:
Post a Comment