HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, May 15, 2022

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, MEJA JENERALI SULEIMAN MZEE AFANYA ZIARA YA KIKAZI MAGEREZA YA SONGWE, MOLLO NA KALILANKULUKULU

 


Kamishna Jenerali wa Magereza, Meja Jenerali Suleiman Mzee akiendesha trekta na akikagua trekta jipya aina ya John Deer HP 110. CGP Mzee amewapongeza Viongozi wa Mkoa wa Katavi na Gereza KalilanKulukulu kwa kununua trekta hilo lililogharimu Tshs 110 milioni.
Moja ya nyumba za makazi ya askari Gereza la Kilimo Mollo, Rukwa ambayo imejengwa kwa njia ya kujitolea. Aidha, Kamishna Jenerali wa Magereza, Meja Jenerali Suleiman Mzee Mzee ameagiza uongozi wa Gereza hilo kuanzisha Kilimo cha umwagiliaji.
Muonekano wa nyumba za Maafisa na askari Gereza Kalilankulukulu mkoani Katavi zikiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi. CGP Mzee amepongeza ujenzi wa nyumba hizo ambazo ni zaidi ya kumi kwa njia ya kujitegemea.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Meja Jenerali Suleiman Mzee akikagua matofali ya "interlocking blocks" yanayotumika katika ujenzi wa nyumba za askari Gereza Kalilankulukulu.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Meja Jenerali Suleiman Mzee akizindua jengo la Ofisi ya Mkuu wa Magereza Mkoani Katavi leo Mei 15, 2022. Jengo hilo limejengwa kwa njia ya kujitegemea.
Muonekano wa jengo la Ofisi ya Mkuu wa Magereza Mkoani Katavi baada ya kuzinduliwa na CGP - Suleiman Mzee.
Maafisa na askari wa Gereza Kalilankulukulu wakionesha shughuli mbalimbali zinazofanyika katika Gereza hilo mara baada ya Mkuu wa Jeshi la Magereza, Meja Jenerali Suleiman Mzee kuwasili katika Gereza hilo kwa ziara ya kikazi leo Mei 15, 2022.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Meja Jenerali Suleiman Mzee(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na maofisa na askari wa Gereza Songwe alipotembelea Gereza hilo. Picha zote na Jeshi la Magereza.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad