HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 12, 2022

Klabu 15 za kuogelea kushiriki mashindano ya FK Blue Marlins

 

Muogeleaji wa klabu ya FK Blue Marlins Loic Makwekwe akishindanai.Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam. Jumla ya klabu 15 zitashiriki katika mashindano ya kwanza ya kuogelea ya

FK Blue Marlins yaliyopangwa kuanza kesho kwenye bwawa la kuogelea la shule ya kimataifa ya FK ya Bahari Beach.

Klabu hizo ni Dar Swimg Club, Mwanza Swim Club, Bluefins, Taliss-IST, Lake Swim Club, Champion Rise Club na Arusha Swim Club.

Klabu nyingine ni Wahoo Zanzibar, MIS Piranhas, Braeburn Sharks, Pigec Swim Club, Train 2 Gain Club, Milestone Swim Club, St Constantine International na wenyeji FK Blue Marlins.

Meneja wa klabu ya FK Blue Marlins Opalina Nanyaro alisema kuwa jumla ya waogeleaji 233 watashindana katika mashindano hayo ambayo yatamalizika Jumapili.

Opalina alisema kuwa zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washindi katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Shoppers Kahawa Cafe, Cool Blue, EFM, Doctors Plaza Polyclinic, PRO Fixers Tanzania, FK International Schools, Viscar Integrated Consulting (TZ) Limited na Coca Cola, GardaWorld.

Kwa mujibu wa Opalina waogeleaji watashindana katika umri tofauti katika staili mbalimbali.

Alisema kuwa pia kutakuwa na mashindano ya waogeaji ya watu wakubwa wenye umri kuanzia miaka 25 na kuendelea au Masters.

Alisema kuwa ‘masters’ wameruhusiwa pia kushindana kwenye kundi la waogeleaji wenye umri wa miaka 15 na zaidi kwa wanawake na kundi la wenye miaka 17 na zaidi kwa wanaume.

Alisema kuwa mbali ya staili tano za kuogelea, waogeleaji hao watashindana katika relei ambayo kwa mtindo wa Individual Medley (IM) na Freestyle. Kwenye IM, waogeaji watachanganya staili nne ambazo ni butterfly, backstroke, breaststroke, na freestyle.
Waogeleaji wa klabu ya FK Blue Marlins katika picha ya pamoja
Muogeleaji wa klabu ya FK Blue Marlins Mischa Ngoshani akichapa maji

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad