Katika kuhakikisha Wakandarasi wadogo na wakati wanajikomboa na hali mbaya ya kuchelewesha miradi wanayopatiwa Suluhisho ya hayo yote limepatikana leo jijini Dodoma
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Bodi ya Wakandarasi nchini, Mkurugenzi wa kampuni ya uuzaji wa magari (trucks) na mitambo ya kutengenezea barabara GF Trucks & Equipment’s Ltd, Salman Karmal aliwataka wakandarasi na Wahandisi nchini kununua magari na mitambo katika kampuni hiyo, kwani wanautaratibu mzuri wa kuwakopesha wakandarasi wadogo na wa kati ambao wana miradi tayari, lakini kutokana na kutokuwa na mitaji wao kama GF wanakitengo maalumu kwa kushirikiana na Tasisi za kibenki kumuwezesha mkandarasi kupata mitambo na magari kwa mashariti nafuu
Pia kampuni hiyo inayojishunghulisha na uuzaji wa Magari ya FAW, HONG YANG na mitambo aina ya XCMG
Mmoja wa Wanufaika wa mpango huo wa kampuni hiyo ambae amefaidika na huduma hiyo ya kukopeshwa vitendea kazi.Mhandisi Baraka Emanueli alisema kupitia kampuni hiyo walianza na 'Tipper' moja na sasa wanamiliki magari matatu, huku walioanza kukopa miaka mitatu iliyopita na kufanikiwa kulipa hatimae sasa hivi wamechukua mashine ya XCMG, hivyo utaratibu huo umewanufaisha wao kwani wakati wanapata tenda ya kuchukua makaa ya mawe hawakuwa na uwezo alimaliza Emanuel.
Waziri wa Ujenzi Makame Mbarawa akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa kampuni ya GfTrucks& Equipments Salman Karmali wakati wa mkutano mkuu wa bodi ya wakandarasi jijini Dodoma
Waziri wa Ujenzi Mhe.Makame Mbarawa akipata maelezo alipotembelea banda la kampuni ya Gf Trucks & Equipments Ltd wakati wa mkutano mkuu wa bodi ya wakandarasi nchini Dodoma .Wakandarasi wakisoma vipeperushi vya kampuni ya Gf ambao ni wadhamini wa mkutano wa bodi ya wahandisi Dodoma
Wakandarasi wakipata maelekezo katika banda la Gf
Thursday, May 12, 2022

Kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Kukopesha wakandarasi Vitendea kazi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment