Na Janeth Raphael - Dodoma
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip
Mpango ameigiza Wizara ya Elimu kuhakikisha inaendelea kujenga
mazingira rafiki yatakayowezesha wanafunzi kupenda zaidi kusoma masomo
ya sayansi na teknolojia pamoja na kuendelea kufanya mapitio ya Sera ya
Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 na kubadilisha mitaala ili kuongeza ubora
wa elimu na mafunzo.
Dkt Mpango ametoa agizo hilo leo Mei
19,2022 wakati akifunga maonesho ya wiki ya ubunifu yanayokwenda
sambamba na Mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia(MAKISATU) kwa
mwaka 2022 ambayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa
Maendeleo(UNDP) kupitia mradi wake wa FUNGUO yaliyofanyika katika uwanja
wa Jamhuri jijini Dodoma.
Makamu wa Rais ameitaka Wizara ya
Elimu kuendelea kutafuta fursa za masomo kwa kwa watanzania katika vyuo
bora duniani katika nyanja za sayansi, teknolojia na tiba kama
ilivyoelekezwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka
2020.
'Wizara inapaswa kuwafuatilia kwa karibu wanafunzi
wabunifu na kuhakikisha wanaendelezwa ili waweze kuwa msaada katika
utatuzi wa changamoto mbalimbali kwa kutumia teknolojia. 'amesema Dkt
Mpango
Hata hivyo amesema kuwa familia zina wajibu wa
kuwahamasisha na kuwatia moyo watoto wanapokuwa na mawazo ya kibunifu
pamoja na kuwaunga mkono katika kupenda elimu ya sayansi.
Dkt Mpango amesema mashindano ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu yanapaswa kufanyika katika mikoa yote.
Aidha
ameiagiza Wizara ya Elimu kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI
kuhakikisha Halmashauri zinatenga maeneo maalum ya kuanzisha vituo vya
ubunifu na atamizi za kisekta kulingana na shughuli za kiuchumi katika
maeneo husika kwa ajili ya kulea vijana wenye ubunifu, ugunduzi na
maarifa asilia.
Katika hatua nyingine Makamu wa Rais ameitaka
taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI) kuhamisha maarifa ya tafiti
katika vitendo. Amewataka kuendelea kutambua mazao yanayoweza
kuwasaidia wakulima hasa wale wa chini kwa urahisi zaidi kulingana na
mvua zinazopatikana katika mkoa husika.
Kwa Upande wake Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa
amesema serikali ya awamu ya sita imedhamiria kwa dhati kuwahudumia
wabunifu ili mawazo na ubunifu uweze kutumika na jamii ya watanzania.
Aidha amezita taasisi zinazohudumia wabunifu kujipanga vizuri pamoja na
kutoa elimu kwao ikiwemo kuwasaidia kulinda hati miliki zao.
Awali
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda amesema
serikali kupitia Buni Hub na DTBI imewezesha kuanzishwa kwa makampuni
zaidi ya 94 yaliotokana na ubunifu na kutoa ajira kwa vijana zaidi ya
30000.
Aidha Prof Mkenda amesema mchango wa kampuni hizo katika
pato la taifa umeanza kuonekana kutoka na baadhi ya kampuni hizo
kuchangia zaidi milioni 500 kwa mwaka kila mmoja.
No comments:
Post a Comment