Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Njombe wakimsikiliza mkuu wa wilaya hiyo wakati wa kikao cha madiwani
Na Amiri Kilagalila, Njombe
MKUU wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa ametoa siku mbili kwa watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Njombe kuhakikisha wanakwenda kupandisha kiwango cha zoezi la anwani za makazi kutokana na hadi sasa kufikia 14% pekee ya uwekaji wa vibao vya barabara na mitaa na kuwa nje ya lengo lililokusudiwa.
Agizo hilo amelitoa katika kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya wakati akitoa salamu za serikali na kuchukizwa na zoezi hilo linaonyesha kusua sua kwenye maeneo mengi na kwamba tayari kuna baadhi ya halmashauri ndani ya wilaya ya Njombe ameagiza kuchukuliwa hatua.
“Bado tuko nyuma,nilikuwa niwachukulie hatua kwa mtendaji ambaye hakijabandikwa kibao hata kimoja kwa kuwa nimefanya hivyo Njombe mjini,sasa hapa nawapa siku mbili nione mabadiriko”Alisema Kissa Kasongwa
“Swala la uwekaji wa Nguzo lengo la kuweka nguzo ni 1980 lakini nguzo zilizosimikwa ni 284 sawa na 14.34% tuko chini”aliongeza Bi Kissa Kasongwa
Awali mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Valentino Hongoli amewaagiza madiwani wote kwenda kuitisha kikao cha dharura cha baraza la maendeleo ya kata (kamaka) ili kujadili utekelezaji wa zoezi hilo la anwani za makazi.
“Kila kata wafanye mikutano ya dharula ya kamaka kwa ajili ya kuharakisha zoezi hili ili twende kasi sawa na serikali yetu”alisema Hongoli
“tarehe ya mwisho ya mkoa ni tarehe 17 kwa hiyo niwapongeze kuweka siku ya kesho na kesho kutwa kuweka mikakati ya kuhakikisha zoezi la uwekaji wa vibao linakamilika ndani ya muda mfupi”alisema Sharifa Nabarang’anya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe
Baadhi ya watendaji wa kata walioshiriki kikao hicho wameeleza hatua waliyofikia ya kutekeleza agizo hilo la serikali ili liweze kwenda kwa muda uliopangwa.


No comments:
Post a Comment