HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 20, 2022

Dalali jela miaka 30 kwa kumbaka binti yake wa miaka 10


 MAHAKAMA ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe imemhukumu kwenda jela kifungo cha mika 30 bwana Dalali Minze Sengerema (36) mkazi wa kijiji cha Ngelenge wilayani humo kwa kosa la kumbaka binti yake mwenye umri wa miaka 10.


Akisomewa hukumu hiyo na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahaka ya Wilaya hiyo Isaac Ayengo imeelezwa kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Novemba 15, 2021 majira ya saa 6 usiku ambapo aliingia chumbani kwa binti huyo na kumbaka huku akimtishia kutosema kwa mtu yeyote na endapo atafanya hivyo atamuua na kumtupa ziwani.

Amesema kwa mujibu wa maelezo ya mke wa mtuhumiwa huyo alieleza kuwa mume wake huyo alitoka nje kujisaidia majira hayo ya usiku lakini akachelewa kuingia ndani naye akaamua kutoka ndipo akakutana na mume wake huyo akitokea chumbani kwa mtoto huyo.

Baadae aligundua kubakwa kwa mtoto wake huyo ndipo akatoa taarifa katika vyombo husika na mtoto huyo alifanyiwa vipimo na kubainika kuingiliwa kimwili.

Awali mwendesha Mashtaka Asifiwe Asajile aliomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa ili iwe fundisho kwake na kwa wote wenye tabia kama hizo .

Hakimu Ayengo amesema amesikiliza ushahidi wa pande zote mbili na huku ushahidi wa upande wa mashtaka ukionekana kuwa na nguvu na kuamua kutoa hukumu hiyo kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 130 (1) (2) (e) na 131 (1) cha Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 marejeo ya 2019.

Aidha katika utetezi wake mtuhumuwa huyo aliiomba mahakama imsamehe kwakuwa ana watoto 13 wenye umri chini ya miaka 18 wanaomtegemea pia na yeye ni yatima.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad