HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 28, 2022

TAS WALAANI MWENZAO KUJERUHIWA MABIBO

 

Na Khadija Kalili
CHAMA Cha Watu wenye Ualbino Tanzania kwa kushirikiana na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRC) wamesema kuwa "Tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kushambuliwa kijana Mohammed Rajabu (18) ambaye ni albino mkazi wa Kata ya Mabibo Jijini Dar es Salaam" alisema Katibu wa Chama Cha Watu wenye Ualbino Tanzania (TAS) Mussa Kabimba alipozungumza na Waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere uliopo ndani ya Hospitali ya Ocean Road.

"Ilitipotiwa kuwa Aprili 25 mwaka huu Mohammed Rajabu alishambuliwa na watu waliokuwa na nia ya kumkata mkono lakini shambulio hilo lilishindikana baada ya vijana waliokuwa maeneo ya jirani walipofanya jitihada za kumuokowa Mohammed ikiwemo kuwarushia mawe watu hao waliokuwa na nia ovu Hali iliyopelekea kufanikiwa kumnusuru kijana huyo asokatwe mkono hivyo waliishia kumjeruhi katika sehemu ya kiganja chake cha mkono na kumsababishia maumivu makali na kisha wahalifu hao walitokomea kusikia julikana" alisema Mussa Kabimba.

"Tunalaani vikali tukio hili ambalo limejitokeza miezi michache baada ya tukio lililopita la kufukuliwa kaburi la mwanaume mwenye Ualbino aliyefahamika kwa jina la Heri Shekighenda lililotokea Novemba Mkoani Tanga.

"Tukio la kujeruhiwa Mohammed linarudisha hofu kubwa kwa sisi watu wenye Ualbino,familia zetu na jamii nzimz kwa ujumla"alisema Katibu huyo wa TASS Kabimba.

Aidha Kabimba alikwenda mbali kwa kusema kusema kuwa TASS wanaliomba Jeshi la Polisi nchini kuchukua hatua za haraka na kufanya upelelezi wa tukio hilo na kuhakikisha wahalifu waluohusika na tukio hilo wanapatikana na kilifiikisha suala hili katika vyombo vya sheria" alisema.

"Kwa kupitia Kamati za Ulinzi na Usalama. kutambua makazi ya watu wenye ulemavu wa ngozi Ualbino waishio katika maeneo Yao na kuimarisha ulinzi katika meneo hayo" alisema Kabimba.

Alisema kuwa kwa kupitia Idara ya Wizara na vitengo husika vinavyosimamia Ustawi wa watu wenye ulemavu nchini kufanya kampeni ya uelelinishaji jamii kuhusu ukweli kuhusu Ualbino na kukanusha Imani zote potofu zilizomo katika jamii ya watanzania hususan kwamba viungo vya mtu mwenye Ualbino huleta utajiri.

Kukamilisha mchakato wa kupitisha Rasimu ya mpango mkakati wa kitaifa wa watu wenye Ualbino (2022-2026)iliyokabidhiwa Ofisi ya Waziri Mkuu Februari mwaka huu.

"Tunamuomba Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa TanzaniaSamia Suluhu Hassan kuingilia kati jambo hili ikiwemo kukemea uovu ,ukatili na mashambulizi yanayofanywa dhidi ya watu wenye Ualbino nchini na kusisitiza matukio haya kushughulikiwa kwa ukamilifu na Vyombo husika" alisema Kabimba.

Aliongeza kwa kutoa r kwa watu wenye Ualbino pamoja na familia zao kuendelea kuchukua tahadhari stahiki kwa ajili ya usalama wao wakati wote ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa Polisi au kwenye vyombo vyenye Mamlaka ambavyo viko karibu mapema iwezekanavyo pindi wanapoona kuna kiashiria chochote Cha uhalifu Ili jitihada za kuzuia zichukuliwe mapema ikiwa ni pamoja na kufanikisha kuwakamata mapema waovu wote wanaojihusisha na vitendo hivi vya kihalifu.

"Mwisho natoa wito kwa vyombo vya habari, Viongozi wa dini, asasi za kiraia pamoja na viongozi wengine wa Serikali kuongeza juhudi katika kutoa elimu kwa jamii kulingana na nafasi walizonazo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad