HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 28, 2022

Ahukumiwa kifungo cha maisha kwa kumbaka mwanaye wa kambo

  

Na Amiri Kilagalila,Njombe
MAHAKAMA ya hakimu mkazi Njombe imemuhukumu Fadhili Ngoho (25) mkazi wa Ulembwe halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe kwenda jela kifungo cha maisha baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka 8.

Mahakama imebainisha kuwa kesi No 193/2020 ilikuwa ikimkabili mshtakiwa Fadhili Ngoho ambaye amehukumiwa kifungo cha maisha baada ya kumbaka mtoto wa miaka 8 ambaye ni mtu na mtoto wake wa kumlea/mtoto wa kambo aliyekuwa akisoma katika moja ya shule ya msingi iliyopo katika kata ya Ulembwe

Inaelezwa kuwa siku hiyo mshtakiwa alimbaka mtoto huyo na kumwambia asipige kelele.

Mnamo tarehe 23/2/2020 mama wa mtoto huyo alimuona mwanae hatembei vizuri ndipo alipomuuliza ana tatizo gani na kisha binti huyo akamwambia mama yake kuwa baba yake wa kambo alimbaka

Tarehe 24/2/2020 mama yake alikwenda kwa mtendaji wa kijiji kutoa taarifa juu ya tukio hilo na alipewa barua ya kwenda polisi, mama huyo alifanya hivyo na taratibu za kumpeleka hospitali mtoto ziliendelea.

Hukumu hiyo imesomwa mbele ya Hakimu mfawidhi wa mkoa wa Njombe Liad Chamshana huku ikiendeshwa na wakili wa serikali Andrew Mandwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad