Serikali
chini ya Benki kuu ya Tanzania (BOT) waliweka kipaumbele utoaji wa
elimu ya fedha kwa Watanzania hususani vijana kwa malengo ya kukuza
jamii iliyo na uelewa na masuala ya fedha.
Kwa kutambua umuhimu
huu, Benki ya NMB kupitia sera ya uwajibikaji kwa jamii, inatoa mafunzo
ya elimu ya fedha kwa makundi tofauti katika maeneo mbalimbali hapa
nchini huku elimu ikielekezwa katika ufunguaji wa akaunti za Benki na
utunzaji wa Akiba kwa manufaa ya baadae.
Katika ziara ya maafisa
wa Benki ya NMB kwa mikoa ya Tabora, Kigoma na Shinyanga, mbali na
kutembelea na kujionea namna Benki hiyo imekuwa chachu ya kukua kwa
sekta ya Elimu na Afya nchini, walitumia fursa hii kutoa Elimu ya fedha
hasa kwa wanafunzi.
Afisa wa benki ya NMB idara ya uwajibikaji
kwa jamii, Aloyce Kikois, aliwasisitiza wanafunzi juu ya uwekaji wa
akiba na kutumia Benki kama sehemu sahihi ya kuhifadhi fedha kwani ni
salama zaidi.
Kwa mujibu wa Meneja wa Benki ya NMB idara ya
Uwajibikaji kwa jamii, Lilian Kisamba alisema, Benki ya NMB tayari
imetoa mafunzo hayo katika maeneo mbalimbali nchini huku zaidi ya
watanzania 80,000 wakinufaika na elimu hii hasa katika ulimwengu wa sasa
wa kiteknolojia
Thursday, April 28, 2022

NMB YAIPA KIPAUMBELE ELIMU YA FEDHAKWA VIJANA NCHINI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment