Serikali
ina matarajio makubwa ya utekelezaji wa Miradi ya Kilimo cha
Umwagiliaji kutokana na ongezeko kubwa la Bajeti ya fedha za miradi ya
Maendeleo kwa Mwaka wa fedha 2022 – 2023, hatua hii ya Serikali ina
lenga kuongeza uzalishaji wa Mazao ya chakula na Biashara kutokana na
kilimo cha Umwagiliaji.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa
Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Reymond Mndolwa alipokuwa
akizungumza na watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Makao Makuu
jijini Dodoma.
Kufuatia hatua hiyo ya Serikali kuongeza kiasi
hicho cha fedha Shillingi Bilioni 146.5 Katika Sekta ya Kilimo cha
Umwagiliaji Bw. Mndolwa ametumia fursa hiyo kuwaasa watumishi wa Tume ya
Taifa ya Umwagiliaji kupendana kushirikiana, kufanyakazi kwa pamoja
(time work) kwa kuzingatia weledi katika maeneo yao ya kazi.
Amesisitiza kuwa suala la kupendana na kuheshimiana katika Utumishi linaongeza ufanisi katika utendaji kazi na kuleta amani.
“Tuheshimu kila mmoja aliyepo hapa, wote thamani yetu ni moja kwa
sababu wote tunaitumikia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.” Alisisitiza
Bw.
Mndolwa ameongeza kwa kusema kuwa watumishi wanao wajibu wa kuhakikisha
wanatunza mali zote za Tume akitolea mfano magari na Mitambo
inayotumika katika shughuli za ujenzi wa miradi ya Umwagiliaji.
“Nataka
kila mtu ahakikishe anatunza mali ile aliyokuwa nayo” ili iweze
kutusaidia kwa muda mrefu zaidi, itunze ione ni mali yako wewe, usione
ni mali ya umma au serikali, sababu serikali ni mimi na wewe “kwahiyo
naomba wale wanaoendesha vyombo vya Mamlaka na wale wanaovipanda
wavitunze.”
Kikao hicho cha Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji ni cha kwanza mara baada ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais
Samia Suluhu Hassan mapema Mwezi huu.

Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji Bw, Reymond
Mndolwa akifafanua jambo mbele ya watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji alipokuwa akizungumza nao Makao Makuu jijini Dodoma
Baadhi ya
Watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wakimsikiliza Mkurugenzi
wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw, Reymond Mndolwa (Hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na watumishi wa Tume hiyo Makao Makuu jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment