HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 27, 2022

Miili ya watu 9 waliofariki kwa ajali Njombe waagwa,Rais Samia atuma salamu za pole


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu ametuma salamu za pole kwa wafiwa kutokana na vifo vya watu 9 waliofariki kwa ajali ya gari mkoani Njombe.

Akitoa salamu hizo kwa niaba ya Rais katika ibada ya kuaga miili hiyo katika kanisa la mtakatifu Joseph jimbo Katoliki Njombe mkuu wa mkoa wa Njombe Waziri Kindamba ametoa wito kwa waombolezaji kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu.

“Lakini pia napenda kuchukua nafasi hii kutoa salamu za pole kutoka kwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambaye naye ameguswa sana na msiba huu”alisema Waziri Kindamba.

Kwa upande wake mhashamu Askofu John Chrisostom Ndimbo wa jimbo Katoliki la Mbinga na msimamizi wa kitume wa jimbo katoliki la Njombe ametoa shukrani kwa serikali,jeshi la polisi pamoja na madaktari kutokana na ushirikiano mkubwa waliouonyesha katika kipindi hiki kigumu kwao.

“Nikushukuru mkuu wa mkoa ulikuwa mstari wa mbele kwa niaba ya serikali ya Tanzania uliposkia taarifa za ajali hiyo,ukakimbia mahospitalini kuwaona lakini pia ukakimbia katika sehemu ya ajali”alisema mhashamu Askofu John Chrisostom Ndimbo

Watu hao ambao ni kutoka umoja wa vijana Katoliki Njombe (UVIKANJO) walifariki kwa ajali ya gari tarehe 24 katika eneo la Igima kibaoni walipokuwa wakitoka

kutembelea kituo cha kulea watoto yatima kilichopo Ibumila wilayani Njombe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad