Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Gilliard W. Ngewe
akizungumza na wandishi wa habari pamoja na wadau ikiwemo viongozi wa
Chama cha Wamiliki wa Mabasi (TABOA) na Chama cha Wamiliki wa Daladala
(TDA) kuhusu nauli mpya za mabasi ya mijini na Mikoani kwenye mkutano
uliyofanyika leo katika ofisi za Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.
Mamlaka
ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imetangaza nauli mpya za mijini na
mikoani ikiwa ni baada ya kukaa na wadau wa usafirishaji kuona ni namna
gani wataweza kutoa huduma bora kwa wananchi
Akizungumza
na waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri
Ardhini (LATRA) Gilliard W. Ngewe amesema baada ya kufanya ukokotoaji
kwa mujibu wa SHERIA ya LATRA ya mwaka 2019 na kanuni zake za mwaka 2020
Mamlaka imeridhia na kujiridhisha pia kuweza kuongeza nauli za mikoani
na mijini.
Amesema
mabasi ya kwenda mikoani kwa daraja la kawaida limeongezeka kwa
shilingi 4.40 sawa na asilimia 11.92 ambapo viwango vya kikomo vya
zamani kwa abiria kwa kilometa moja ilikuwa ni shilingi 36.89 na sasa
viwango ambavyo Mamlaka imeridhia kwa abiria kwa kilometa moja inakuwa
shilingi 41.29.
Pia
amesema mabasi ya kwenda mikoani kwa daraja la kati limeongezeka kwa
shilingi 3.66 sawa na asilimia 6.88 ambapo viwango vya kikomo vya zamani
kwa abiria kwa kilometa moja ilikuwa ni shilingi 53.22 na sasa viwango
ambavyo Mamlaka imeridhia kwa abiria kwa kilometa moja inakuwa shilingi
56.88.
"Viwango
vya nauli kwenye barabara za vumbi itakuwa na ongezeko la asilimia 25
ya daraja la kawaida kwa barabara ya lami ambayo ni sawa na shilingi
51.61 kwa abiria kwa kilometa. Alisema Ngewe
Ameongeza
kuwa mabasi ya mijini nauli imeongezeka shilingi 100 kama nauli ya
mwanzo abiria alikuwa analipa shilingi 400 sasa atalipa shilingi 500 na
kama abiria mwanzo alikuwa analipa nauli ya shilingi 750 sasa utalipa
shilingi 850.
Awamewasisitiza
watoa huduma kwa kuzingatia kanuni ya 19 ya tozo ya LATRA ya mwaka 2020
inayowataka kutoa matangazo ya nauli mpya kwa siku kumi na nne kabla ya
kuanza kutumia nauli mpya kupitia vyombo vya habari vinavyoweza
kuwafikia watu wengi nchini
No comments:
Post a Comment