HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 4, 2022

Benki ya CRDB yapata ugeni kutoka Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo ya Afrika Mashariki

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kulia) akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mkuu wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo ya Afrika Mashariki (EACCIA), Charles Kahuthu wakati ujumbe wa viongozi wa chemba hiyo kutoka nchi sita ulipomtembelea ofisini kwake. Ujumbe huo uliambatana na Rais wa Baraza la Biashara Barani Afrika Dr. Amany ASFOUR (kushoto). Ujumbe huo umepongeza mkakati wa Benki ya CRDB wa kupanua biashara yake katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki ambao unachochea utekelezaji wa mkataba wa Makubaliano ya Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AFTA). Benki ya CRDB ni mmoja wa wadhamini wakuu wa Wiki ya Biashara na Viwanda Afrika Mashariki (EATIW) 2022 ambayo kilele chake ni leo tarehe 1 Aprili 2022. 
Rais wa Baraza la Biashara Barani Afrika Dr. Amany ASFOUR (kushoto) akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati wajumbe wa viongozi wa Chemba za Biashara tofauti sita (Misri, Zambia, Botswana, Rwanda, Burundi, Ethiopia na Uganda) walipotembelea makao makuu ya Benki ya CRDB. Wengine pichani ni, Mkurugenzi Mkuu wa EACCIA, Charles Kahuthu, na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Congo, Jessica Nyachiro. Ujumbe huo umepongeza mkakati wa Benki ya CRDB wa kupanua biashara yake katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki ambao unachochea utekelezaji wa mkataba wa Makubaliano ya Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AFTA). Benki ya CRDB ni mmoja wa wadhamini wakuu wa Wiki ya Biashara na Viwanda Afrika Mashariki (EATIW) 2022 ambayo kilele chake ni leo tarehe 1 Aprili 2022.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad