HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 4, 2022

AJENDA 10/30 KILIMO BIASHARA


Na Evelyne Mpasha TARI, Dodoma

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amefurahishwa na bidhaa pamoja na teknolojia mbalimbali zilizotokana na matokeo ya utafiti na kuiagiza TARI kupeleka matokeo ya utafiti na teknolojia bora kwa wakulima na wadau wa kilimo il kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao badala ya kukaa na tafiti hizo ofisini.


Agizo hilo amelitoa wakati alipotembelea banda la TARI na kujionea teknolojia mbalimbali za mazao zilizofanyiwa utafiti wakati wa uzinduzi wa ugawaji wa vitendea kazi kwa Maafisa ugani kilimo nchini. Vifaa vilivyogawiwa ni pamoja na pikipiki 600, simujanja, visanduku vya ufundi "extension kit" na vifaa vya kupimia afya ya udongo.

Ugawaji wa vifaa hivyo kwa maafisa ugani kutaongeza chachu na hamasa kwa maafisa ugani kilimo zaidi ya 7,000 waliopo nchini kuwahudumia wakulima kwa urahisi ili kuleta mapinduzi katika sekta ya kilimo.

Aidha, Mhe. Rais ameitaka Wizara ya Kilimo kuweka msukumo kwenye uzalishaji wa mazao ya chakula na kuwa ya kibiashara yakiwemo mazao ya kimkakati ili kukidhi mahitaji ya ndani na ziada kwa ajili ya soko la nje.

Awali katika taarifa yake, Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe alimshukuru Mhe. Rais kwa kuiongezea Wizara yake bajeti kutoka shilingi bilioni 7 hadi kufikia shilingi bilioni 11na kwamba yeye na timu yake Wizarani wamejipanga kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo ili kujihakikishia usalama wa chakula, lishe bora, ajira inayotokana na kilimo kupitia mnyororo wa thamani.

Kwa mujibu wa Mhe. Rais, Sekta ya Kilimo ieendelea kukuza uchumi na kuleta maendeleo kwa taifa abapo huchangia asilimia 65 ya malighafi za viwandani na asilimia 61.1 kutoa ajira kwa Watanzania.

Uamuzi huu wa Wizara ya Kilimo kugawa vitendea kazi kwa maafisa ugani kilimo nchini ni moja ya utekelezaji wa Maazimio ya Malabo za kuinusuru Afrika na njaa na kuondokana na umasikini wa chakula ifikapo 2035 kwa kuwekeza nguvu zake kwenye uwekezaji kabambe wa sekta ya kilimo.

Tanzania ni wanachama wa AU, ambao kwa pamoja walikubaliana kuweka asilimia 10 za bajeti za Serikali za nchi zao kwenye kilimo ili kuwa na uwekezaji endelevu.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad