Na Mwandishi wetu, Dar
WAZIRI
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata
Mulamula (Mb) amekutana kwa mazungumzo na Mwakilishi wa Heshima wa
Tanzania nchini Czech Bw. Roman Grolig katika Ofisi ndogo za Wizara
Jijini Dar es Salaam.
Katika
mazungumzo yao, viongozi hao wamekubaliana kuimarisha uhusiano baina ya
Tanzania na Jamhuri ya Czech katika sekta za biashara na uwekezaji,
kilimo, elimu na teknolojia.
Balozi
Mulamula aliwakaribisha wawekezaji kutoka Czech kuwekeza nchini pamoja
na kutia mkazo wa kuimarisha zaidi ushirikiano kati ya Tanzania na
Czech.
Kwa
upande wake, Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Czech, Bw. Grolig
amesema ataendelea kuwahamasisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka
Czech kuja kuwekeza Tanzania kwani ni sehemu salama ya kuwekeza.
“Jamhuri
ya Czech imedhamiria kuongeza ushirikiano na Tanzania na katika
kutimiza azma hiyo, wafanyabiashara na wawekezaji wameonesha nia ya
kuwekeza katika viwanda vya kutengeneza ndege ndogondogo Pamoja na
magari makubwa hapa Tanzania,” amesema Bw. Grolig
Pia
ameongeza kuwa kwa sasa Czech ipo katika mchakato wa kuanzisha safari
za ndege za moja kwa moja hapa nchini Tanzania ili kuwawezesha
wawekezaji na wafanyabiashara kusafiri kwa urahisi kuja Tanzania
kutafuta fursa za uwekezaji,” amesema Bw. Grolig.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata
Mulamula akiongea na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Czech Bw.
Roman Grolig katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mwakilishi
wa Heshima wa Tanzania nchini Czech Bw. Roman Grolig akimfafanulia
jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Liberata Mulamula walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za
Wizara Jijini Dar es Salaam
Mazungumzo
baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Liberata Mulamula na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini
Czech Bw. Roman Grolig yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini
Dar es Salaam.
Mazungumzo
baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Liberata Mulamula na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini
Czech Bw. Roman Grolig yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini
Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata
Mulamula katika picha ya pamoja na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania
nchini Czech Bw. Roman Grolig
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata
Mulamula na Mwakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Czech Bw. Roman
Grolig katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani
Dkt. Abdallah Possi, Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Balozi
Swahiba Mndeme na Afisa mambo ya Nje kutoka Wizarani, Bibi Kisa Mwaseba.
Kushoto mwa Bw. Grolig ni maafisa alioambatana nao kutoka Jamhuri ya
Czech
No comments:
Post a Comment