Charles James
WAZIRI
 wa Katiba na Sheria George Simbachawene, amesema serikali ya Tanzania 
ipo katika mchakato wa kurudi kuwa wanachama wa Mahakama ya Afrika baada
 ya kujitoa kwa muda sasa kutokana na sababu mbalimbali.
Simbachawene,
 alibainisha hayo juzi mara baada ya kikao cha pamoja na viongozi wa 
Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania (THRDC) kilichofanyika 
katika ofisi za wizara ya Katiba na Sheria Mtumba jijini Dodoma.
Alisema, suala la Tanzania kujitoa katika Mahakama ya Afrika, zilikuwepo sababu lakini haziwezi kuwa za kudumu.
 
Waziri Simbachawene, alieleza kuwa mazungumzo yanaendelea ndani ya serikali na anaamini nchi itarudi tena katika Mahakama hiyo.
 
"Mahakama
 hii ipo Tanzania, inakuwa si vizuri sana kama tena sisi Watanzania 
tutakuwa hatupo kwenye hii Mahakama tupewe muda, mchakato unaendelea 
nina imani si muda mrefu maamuzi yatatolewa na serikali"alisema 
Simbachawene
 
Aidha, alisema Tanzania ni nchi ambayo inatambua, 
inaheshimu, inatunza  na kulinda haki za binadamu, na itaendelea 
kushirikiana na wadau wa masuala ya Haki za Binadamu.
 
“Katika 
mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia ameonyesha nia ya kutunza haki 
maeneo ambayo yameonyesha kuwa na shida katika maeneo ya haki za 
binadamu anafanya hivyo kwa vitendo, pamoja na nadharia.
 
“Wizara
 ya Katiba na Sheria imefurahi kuona mpo na itaendelea kushirikiana na 
nanyi katika kila jambo ambalo mtapenda tushirikiane." alisema 
Simbachawene
 
Pia, aliwataka Watetezi wa Haki za Binadamu nchini 
kuhoji na kuzungumza na wizara, kuliko kupeleka katika majukwaa ya 
kimataifa na kuiondolea heshma nchi.
 
Vilevile, alisema Wizara 
itashiriki kwa pamoja na AZAKI katika majukwaa ya kimataifa ili 
kuhakikisha Tanzania inajengwa kwa mashirikiano thabiti na yenye tija 
kati ya pande zote mbili.
 
Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa, 
katika kikao hicho alitaja baadhi ya maeneo ambayo yanaweza kufanyiwa 
maboresho na wizara ikiwemo  kuwa na utataratibu mzuri wa kufahamu, 
kuripoti na kutambua kazi za watetezi wa Haki za Binadamu kama wadau 
muhimu wa wizara hiyo.
 
“Pia, kufanyika kwa maboresho katika 
maeneo ya utoaji wa msaada wa kisheria,uboreshwaji wa mifumo ya utoaji 
haki nchini,maboresho ya baadhi ya sheria ikiwemo sheria ya NGO, hasa 
katika upatikaji wa vibali vya tafiti inayoyataka mashirika kupitia 
TAMISEMI ili kupata pamoja na sheria zingine,ushiriki wa wizara katika 
mikutano na majukwaa ya kimataifa,Tanzania kurudi katika mahakama ya 
Afrika Mashariki”alisema
 
Pamoja na meneo hayo ya maboresho THRDC
 pia imetoa mapendekezo ya kufanyiwa kazi na wizara katika kuboresha 
shughuli za utetezi wa Haki za Binadamu nchini.
 
 Mapendekezo 
hayo ni pamoja na kuboreshwa kwa mfumo wa utekelezaji (Human Rights 
Enforcement Mechanism - BRADEA) sheria iliyokuwa inaweka utaratibu wa 
kulinda haki za kikatiba.
 
Olengurumwa, alisema mabadiliko 
yaliyofanyika yameweka vikwazo vingi kwa mtanzania mmoja mmoja au 
taaisisi zao kutekeleza agizo la ibara ya 26/2 ya kulinda katiba.
 
“Kumekuwa
 na vigingi vingi ambavyo tunaweza kufanya majadiliano na  maboresho 
kupitia wizara hii ambavyo  yatatoa fursa ya watanzania kwenda moja kwa 
moja na Taasisi za Haki za Binadamu kwenda mahakamani kulinda na kutetea
 haki za Binadamu kupitia mlango wa kikatiba.
 
“Kuwepo kwa 
National human rights Action plan (Mpango wa Taifa wa Haki za Binadamu, 
serikali iangalie namna ya  kuharakisha kukamilika kwa  mchakato huo ili
 kuwa na andiko litakalotoa mwongozo utawaunganisha wadau wa haki za 
Binadamu na serikali."alisema Olengurumwa
 
Hata hivyo, alisema 
kuwepo na Sera ya Haki za Binadamu ambayo inaweza kutoa mwongozo kwa 
taasisi binafsi na serikali kuhusiana na masula ya haki za binadamu. 
 
“Sera
 hii itawatambua na kuwalinda watetezi wa Haki za Binadamu. Hii ni 
kuwawezesha Wadau pamoja na serikali wawe na uelewa wa pamoja wa maswala
 ya utetezi na Watetezi wa Haki za Binadamu nchini. 
 
“Kumekuwa 
na changamoto za utekelezaji wa maamuzi wa Mahakama za ndani na nje hasa
 katika maeneo ya access to justice katika kesi za Haki za Binadamu, 
lazima uje Dar es Salaam. Tunapendekeza serikali iruhusu kila high kort 
yenye hadhi ya Mahakama Kuu iwe na uwezo wa kusikiliza kesi hizo katika 
Mikoa kesi hizo ziliporipotiwa." Alisema Olengurumwa.
Waziri wa Katiba na Sheria George Simbachawene akikabidhiwa mapendekezo na Viongozi wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, THRDC ofisini kwake Mtumba Jijini Dodoma.
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania THRDC, Onesmo Olengurumwa akizungumza katika kikao baina ya Mtandao huo na Waziri wa Katiba na Sheria, George Simbachawene jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria, George Simbachawene akiwa katika picha ya Pamoja na Viongozi wa Wizara hiyo ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma.
 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment