HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 28, 2022

Wafanyakazi NIC waanzisha siku ya kujenga mahusiano ya ufanisi kazini


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Bima (NIC)Dk.Elirehema Doriye akizungumza na wafanyakazi wa Shirika hilo katika Siku ya Coporate Day yenye lengo ya kukuza mawasiliano ubunifu wakiwa kazini ,jijini Dar es Salaam.

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Dk..Elirehema Doriye akiwa katika picha ya pamoja na Waratibu na Wazeshashaji wa  wafanyakazi wa shirika hilo katika Siku ya Coporate Day iliyifanyika Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Bima (NIC) Dk..Elirehema Doriye akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo katika Siku ya Coporate Day iliyifanyika Jijini Dar es Salaam.
Picha mbalimbali zinazoonyesha mshikamano na mawasiliano wakiwa kazini huku baadhi wakiwa wamebana lengo ni kuonyesha wakati wa kazi wengine wanaweza kuumia kwa lengo ya wenzake wafanikishe kazi
Meneja Rasimali Watu wa Shirika la Taifa la Bima (NIC), Veneranda Mpaze akizungumza umhimu wa siku ya Coporate Day kwa wafanyakazi kuwa panoja katika kufanya ubunifu wa utoaji huduma ,jijini Dar es Salaam
.

*Dk.Doriye aamini mapinduzi ya mafanikio katika NIC

Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv 
WAFANYAKAZI Wafanyakazi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) wamekutana pamoja nje ya eneo la kazi kujadili ni namna gani wanaweza kuendeleza ushirikiano katika kazi ili wateja wao waweze kufurahia huduma zinazotolewa na Shirika hilo kwa kupata huduma iliyo bora zaidi kwa kuamini mteja ndio mtu mhimu katika wao kufanya kazi.

Kukutana pamoja kwa wafanyakazi ni kutaka kuweka mapinduzi ya mafanikio kwa shirika ambayo inaonyesha kuanzishwa kwake kunakuwa na mafanikio endelevu.

Akizungumza katika siku hiyo Muhimu ambayo wameiandaa kwa kuipa jina la "NIC Coperate Day" Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dk.Elirehema Doriye amesema wanatakiwa kuwa nguvu ya pamoja 'Team Work' kitu ambacho wanatakiwa kukijenga wakiwa ndani nje ya makazini mwao ili huduma wanayoitoa iwe bora kutegemeana na ushirikiano ambao umejengwa wenye lengo wa kutoa huduma bora kwa wateja wakiamini NIC ni shirika la kutoa huduma zilizo bora.

"Tunapokuwa na mahusino mazuri sisi maan yake pia tunaweza kusaidiana, kushauriana lakini kwa pamoja tunaweza kuweka mawazo ambayo yanaweza kuleta chachu ya ubunifu wrnye kufanya shirika liendelee kukua kila siku" amesema Dk. Doriye.

Amesema siku hii iwe mwanzo wa namna wanavyofungua mawasiliano katikati yao kwasababu dhumuni kubwa la kukutana na kushiriki katika shughuli mbalimbali ili waweze pia kuwasiliana kutokana sio wote wanatoka sehemu moja bali wengini wa wako katika mikoa mingine ambapo kukutana kwao ni kuwa daraja ya kuwa na mawasiliano ya kusaidia shirika kusonga mbele.

Kwa upande wake Meneja wa Rasilimali Watu na Utawala NIC, Bi.Veneranda Mpaze amesema wamekutana kwaajili ya kuhamasisha afya ya akili na mwili pamoja na kusapoti mpango wa kitaifa wa kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza mahala pa kazi pamoaja na kujenga nguzo imara ya kutoa huduma bora

Aidha amesema wafanyakazi hutegemeana hivyo kukutana kwao kuna jenga mawasiliano mazuri na kuweza kuwahudumia wateja wao kwa kupata huduma bora na zenye viwango kutoka NIC"Sisi Ndiyo Bima."

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad