HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 28, 2022

Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu yatoa elimu juu ya utuzaji wa vyanzo vya maji


Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa wa Mwanagati akionesha uharibifu wa vyanzo vya maji katika Mto Nkerenzange unaofanywa wananchi kwa kuendesha kilimo nje ya taratibu za kiserikali.
*Kaimu Afisa Maji Msaidizi Dar es Salaam Halima:Mito sio sehemu.salama ya kuendesha shughuli za Kibidamu

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
BODI ya Bonde la Wami/Ruvu kwa kushirikiana wadau Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) wametembelea Mito katika jiji la Dar es Salaam kuangalia shughuli za kibidamu zinazofanyika katika Mito hiyo ambazo zinaharibu vyanzo vya maji.

Akizungumza katika ziara ya kutebelea mito katika jiji la Dar es Salaam Kaimu Afisa Maji Msaidizi wa Bonde la Wami/Ruvu Dar es Salaam Halima Faraj amesema kuwa kuendelea kufanyika kwa shughuli za kibidamu katika mito ni kinyume na sharia ya usimamizi wa rasilimali za maji.

Amesema kuwa wananchi waliopo katika vyanzo vya maji wanatakiwa kuacha kufanya shughuli zoozte katika mito na kufanya kazi mbadala kwani vyanzo vya maji hivyo vikifa ni janga kwa watukutokana na umhimu wa maji katika shughuli za kibidamu .

Halima TBL kushirikiana na bonde sio kwa bahati mbaya ni kutokana na kuthamini maji kwani uzalishaji wao unategemea asilimia 100 ni maji hivyo maji kwao wanayaona ni dhahabu na vyanzo vya maji vikichafuliwa hawawezi kuzalisha.

“Hatuwezi kuendelea kuruhusu shughuli za kibidamu kwani madhara yake ni makubwa kwa jamii hivyo wananchi watake wasitake waachane na shughuli hizo na tukiwa wasimamizi wa sharia lazima tufanye hivyo ukiwa kukamatwa kwa wataokutwa katika mito ikiwa pamoja na kutozwa faini na wakati mwingine ni kifungo”amesema Halima

Aidha amesema kuwa serikali imewekeza katika sekta ya maji kuhakikisha wananchi wanapata maji katika maeneo yote hivyo hakuna sababu ya wananchi kufanya shughuli za kibidamu katika vya nzo vya maji ikiwemo mito.

Amesema katika mto Msimbazi kuna shughuli zingine zinafanyika za kuchafua mito kwa kulundika takataka za majumbani na kusababisha maafa wakati wa mvua ambapo madhara hayo kuwarudia wao wenyewe tukiwa wasimamizi tutasimamia mpaka mwisho watu kukoma katika utupaji wa taka katika mito

Nae Meneja Mazingira na Usalama mahala Pa Kazi wa TBL Revocatus Rutakwa amesema kuwa maji ni bidhaa muhimu hivyo wanashirikiana na serikali katika kuendelea kulinda vyanzo vya maji kwa kuhakikisha kila tone la maji linasimamiwa.

Amesema kuwa wananchi wakiachana na shughuli za kibidamu katika mito itafanya kila mwananchi kuwa na uhakika wa maji pamoja na wenye viwanda ikiwemo TBL kunufaika kwa kuendelea kuzalisha bidhaa za viywaji.
Picha ya pamoja mara baada kuweka bnago linalokataza kufanyika kwa shughuli za kibidamu kwa wananchi wa Vingunguti walio kandokando ya Mto Msimbazi.
Kaimu Afisa Maji Msaidizi wa Bonde la Wami/Ruvu Halima Faraji akizungumza wanachi wa Vingunguti walio pembezoni mwa Mto Msimbazi kuhuisiana na uchafuzi wanaofanya Mto huo na kusababisha mafuriko kila wakati wa masika ,jijini Dar es Salaam.
Kaimu Afisa Maji Msaidizi wa Bonde la Wami/Ruvu Halima Faraji akizungumza wanachi wa Vingunguti walio pembezoni mwa Mto Msimbazi akionesha namna shghuli za kibidamu zinavyoharibu Mto huo na huo na kusababisha mafuriko kila wakati wa masika ,jijini Dar es Salaam.
Meneja Mazingira na Usalama Mahala Pa Kazi wa TBL Revotus Rutakwa  akizungumza umhimu wa wananchi wa kutunza vyanzo vya maji kutokana umhimu wa uzalishaji wa viywaji katika TBL ,jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad