HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 8, 2022

NBAA YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 2022

 


Tarehe 8 Machi ya kila mwaka ni Siku ya wanawake duniani, ambapo siku hii inataka kukumbushia na kutafakari juu ya matokeo ya kisiasa, kijamii, kiuchumi waliyofikia wanawake na msimamo wao imara katika ngazi ya kijamii kwa ujumla.

Katika kuadhimisha siku hiyo Wanawake wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) wameshiriki maadhimisho hayo yaliyofanyika leo katika viwanja vya Uhuru Mkoani Dar es Salaam. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni "Kizazi cha Haki na Ustawi kwa Maendeleo Endelevu"

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, Mwenyekiti wa Wanawake wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA, Irene Mutagaywa amewataka wanafunzi walioko mashuleni kujikita katika kutengeneza ndoto zao kwa kusoma kwa bidii ili kuwa sehemu ya wanawake waliofanikiwa katika nyanja mbalimbali hapo baadaye.

Pia amesema mafanikio yoyote yanayoonekana hapa nchini na duniani kote kwa kiasi kikubwa pia yamechagizwa na uwepo wa wanawake huku pia akimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa rais mwanamke wa kwanza hapa nchini Tanzania na pia kwa kuendelea kuwaamini wanawake katika nafasi mbalimbali za kiuongozi kwenye Serikali yake.

Siku ya wanawake duniani ilianza kutokana na jitihada za wanawake 15,000 mwaka 1908 walipoandamana mjini New York Marekani wakidai kupunguziwa muda wa kufanya kazi, ujira wa kuridhisha na haki ya kupiga kura. Kilikuwa ni chama cha kisoshalisti cha Amerika kilichotangaza kuwa ni siku ya kwanza ya kitaifa ya wanawake, mwaka mmoja baadaye. Wazo la kuwa siku ya kimataifa lilianzishwa na mwanamke kwa jina la Clara Zetkin. Yeye alipendekeza wazo hilo mwaka 1910 katika mkutano wa kimataifa wa wafanyakazi wanawake huko Copenhagen Denmark.

Picha mbalimbali  za matukio za baadhi ya wafanyazi wanawake wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) katika maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani yaliyofanyika leo Machi 08, 2022 katika viwanja vya Uhuru jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad