MAHAKAMA
Kuu, Divisheni ya Rushwa na Ujumumu Uchumi, Dar es Salaam imemuachia
huru Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu baada ya
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kwa kuwasilisha hati ya kutakuwa na
nia ya kuendelea na mashtaka dhidi yao.
Mbowe
na wenzake, Adam Kasekwa, Halfani Bwire na Mohamed Ling’wenywa
waliokuwa makomandoo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
wameachiwa huru leo Machi 4, 2022 na Jaji Joachim Tiganga.
Mapema
kesi hiyo iliitwa mahakamani hapo kwa ajili ya washtakiwa kuanza
kujitetea lakini Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando alieeleza
mahakama kuwa DPP amewasilisha hati (Nolle) kuwa hana nia ya kuendelea
na mashtaka dhidi ya washtakiwa.
No comments:
Post a Comment