HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 4, 2022

MAJENERALI WASTAAFU WAAGWA, WALIOBAKI WAASWA KUWA NA NIDHAMU YA KUTOSHA

Na Karama Kenyunko Michuzi TV
MKUU wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Generali Venance Mabeyo amewaasa wanajeshi kuwa na nidhamu ya kutosha kazini ili waje kuwa na mwisho uliotukuka.

Mabeyo ameyasema hayo leo Machi 4, 2022 wakati wa hafla ya kuwaaga Majenarali wastaafu wanne na mabrigedia Jenerali wastaafu wanne katika viwanja wa Twalipo Mgulani, Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya hafla hiyo, Mabeyo amesema, ni heshima kubwa kuwaaga mwenzao hao ambao wamefikia kikomo cha utumishi wao jeshini ambapo wametumikia kwa zaidi ya miaka 30 huku wakiacha alana ya utumishi uliotukuka

Amesema, ni mstaafu, aliyestaafu kwa heshima pekee ndio hufanyiwa sherehe za kuagwa kiheshima lakini huwezi kufanyiwa sherehe za kuagwa kama ulifukuzwa kazi ama ulikuwa na utumishi usiotukuka.

"Huwezi kuitwa msataafu uliyestaafu kwa heshima ukafanyiwa sherehe kama hizi kama unakuwa umefukuzwa, ukiwa umefukuzwa huwezi kufanyiwa sherehe kama hizi, sherehe kama hizi maana yake utumishi wako ulikuwa wa kutumainiwa na kila mmoja na watu wote wangependa iwe hivyo." Amesema Mabeyo.

Amesema ni heshima kulitumikia Taifa kwani hata wastaafu hao wakirudi uraiani wanaenda kushirikiana na jamii ambayo nayo itakuwa na matumaini kwamba wanamwenzao ambaye alikuwa analitumikia Jeshi la wananchi wa Tanzania.

Siku hii ni ya heshima kubwa kwa wenzetu katika utumishi wao Jeshini, sherehe ya leo inaonyesha kuwa wamestaafu kwa heshima, wamestaafu katika umri tofauti tofauti na muda walioutumikia jeshi tofauti tofauti lakini maofisa hawa walikuwa na utumishi uliotukuka".

Amesema, kustaafu kwa heshima maana yake ni kuwa utumishi wao ulikuwa umetukuka, ambapo unalitumikia Jeshi kwa miaka 20 mfululizo au zaidi ya hapo. Hivyo hawa wanatoka kwa heshima hiyo na wanastahili pongezi waliyoipata.

Hata hivyo Mabeyo ameelezea utaratibu wa Jeshi ni kwamba mstaafu anapokuwa ameondoka jeshini anakuwa bado akitambulika kwa miaka mitatu ili wakati wowote linapotokea akihitajika kurudi ndani ya jeshi basi anarudi mara moja yaani wanakuwa ni wanajeshi wa akiba.
Maofisa walioagawa leo ni, Meja Jenerali George William Ingram, Meja Jenerali Alfred Fabian Kapinga, Meja Jenerali Kaisy Philip Njelekela na Meja Jenerali Henry Sweke Kamunde.

Wengine ni, Brigedia Jenerali Regnald Kasmiri Kapinga, Brigedia Jenerali Zaharani Saidi Kiwenge, Brigedia Jenerali Charles Mutembei Buberwa, Brigedia Jenerali Marianus Gotlieb Mhagama.
Baadhi ya wastaafu wa Jeshi la Tanzania wakiwa kwenye gari maalumu kwaajili kuonesha utumishi uliotukuka leo Machi 4, 2022 wakati wa hafla ya kuwaaga Majenarali wastaafu wanne na mabrigedia Jenerali wastaafu wanne katika viwanja wa Twalipo Mgulani, Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.












































No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad