HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, March 27, 2022

DKT. STERGOMENA AFUNGUA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI SHIRIKA LA MZINGA

Picha ya Pamoja waziri wa Ulinzi na JKT Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) na Ujumbe wake akiwa na viongozi wa Shirika la Mzinga pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Mzinga kwenye viwanja vya Hoteli ya Tanga Beach ResortWaziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,  Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) akitoa Hotuba ya Ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Mzinga ufunguzi huo ulifanyika kwenye Hoteli ya Tanga Beach Resort Jijini Tanga.

Meneja Mkuu wa Shirika la Mzinga Brigedia Jenerali Seif Hamisi akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rami Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi na Keshi la Kujenga Taifa kwenye ufunguzi wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Mzinga tukia lililofanyika Tanga Beach Resort Jijini Tanga.
Picha ya Pamoja waziri wa Ulinzi na JKT Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) na Ujumbe wake akiwa na viongozi wa Shirika la Mzinga pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Mzinga kwenye viwanja vya Hoteli ya Tanga Beach Resort

WAZIRI wa Ulinzi na JKT, Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) amefungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Shirika la Mzinga - Morogoro. Kikao hicho cha siku moja kimefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort jijini Tanga.

Agenda za kikao hicho ni pamoja na kupitia Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti kwa Kipindi cha Nusu Mwaka (Julai 2021– Disemba 2022), Maoteo ya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 pamoja na dondoo kutoka kwa wajumbe.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho, Dkt. Stergomena aliwakumbusha wafanyakazi hao kujiwekea mipango na mikakati. Mipango itasaidia kujua nini cha kufanya, muda gani na rasilimali gani zinahitajika. Aidha, aliwahakikishia kuwa Wizara itafanya kila liwezekanalo kuwawezesha ili waweze kufikia malengo. 

“Pamoja na mafanikio yaliyopatikana upo umuhimu wa kuwa na mipango na mikakati madhubuti itakayoliwezesha Shirika kuhakikisha kuwa ufanisi na mafanikio ni endelevu. Ili jambo liweze kufanikiwa lazima muda wote kuwe na mipango mkakati ya kufanya hivyo. Kwa sababu mipango hiyo inakuwezesha kujua unahitaji kufanya nini, muda gani na unahitaji rasilimali gani na inakuwezesha kujipanga,ili hata sisi kama tunahitajika kuwasaidia tuajua mapema kuwa ni kitu gani kinahitajika, ikiwa ni pamoja kubuni miradi”, alisema.

Kuhusu kufanya utafiti, Dkt. Stergomena amebainisha kuwa utafiti ni mingoni mwa majukumu ya msingi ya Shirika. Kwa maana hiyo, wanatakiwa kuibua tafiti mbalimbali kwa kuwa bila kufanya utafiti maendeleo yatasuasua.

“Utafiti ni miongoni mwa  mwa majukumu ya msingi ya Shirika la Mzinga , kwa  muktadha huo, nachukua nafasi hii kuwakumbusha kuibua na kuendeleza tafiti mbalimbali zitakazoliletea tija Shirika, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Jeshi la Kujenga Taifa, Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama na taifa kwa ujumla. Bila utafiti, iwe ni taasisi, iwe ni taifa maendeleo huwa yanasuasua”, alibainisha.

Tija ya Shirika inapatikana kwa kuwa wafanyakazi kuwa wanakuwa ni sehemu ya maamuzi. Kwa maana hiyo, iangaliwe namna bora ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi. Aidha kuwepo na mpango wa mafunzo na kuongeza tija kwa kuzingatia dira na dhima  ya kuanzishwa kwa Shirika. 

Akitoa taarifa ya Shirika, Meneja Mkuu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo, Brigedia Jenerali Seif Athuman Hamisi amesema Shirika la Mzinga ni mojawapo ya mashirika chini ya Wizara ya Ulinzi na JKT, lililoanzishwa tarehe 13 Septemba 1974.

“Shirika la Mzinga ni mojawapo ya mashirika ya JWTZ  chini ya Wizara. Ni Shirika la kimkakati linalozalisha mazao ya msingi. Kwa maana hiyo, Shirika hili ni muhimu sana. Mwaka 2024 litakuwa linatimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake kama Shirika la Umma”, alisema.

Kuhusu uzalishaji Brigedia Jenerali Hamisi amesema kuwa muda mrefu tangu kuanzishwa kwake Shirika halikuweza kuzalisha kwa tija kwa kuwa uzalishaji ulishuka, lakini jitihada zimefanyika ambapo kwa miaka miwili mfululizo uzalishaji umeongezea hadi kufikia asilimia 97. Ameahidi kuwa mafanikio hayo yatalindwa na kudumishwa. 

“Tuapoazimisha miaka 50 ya Shirika tutahakikisha kuwa maadhimisho hayo yanaendana na tija itakayokuwa imepatikana kwa muda huo. Utendaji wake kiuzalishaji kwa muda mrefu ulishuka kama ilivyokuwa kwa mashirika mengine ya umma. Lakini kwa sasa baada ya jitihada kubwa kufanyika, hadi kufikia mwezi Februari 2022 uzalishaji umeongezeka hadi kufikia asilimia 97”, alisema.

Vikao vya mabaraza ya wafanyakazi ni utekelezaji wa takwa la kisheria ambalo chimbuko lake ni Tamko la Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius K. Nyerere (Tamko Na. 1 la Mwaka 1970) na Sheria nyingine za kazi za nchi yetu na zile za kimataifa zinazohimiza ushirikishwaji wa wafanyakazi katika kufanya maamuzi mbalimbali kupitia mabaraza ya wafanyakazi. Aidha, Baraza hili ni jukwaa muhimu sana mahali pa kazi kwani ni kiungo kati ya Menejimenti na Wafanyakazi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad