Benki ya NMB
yazindua msimu wa pili wa ‘Umebima’ ikiwa ni kampeni ya kuhamamisha na
kuelimisha matumizi ya huduma za Bima kwa Wateja wake na Watanzania wote
kwa ujumla.
Kampeni hii ilizinduliwa katika Soko la Karume na
Afisa Mkuu wa Wateja binafsi na biashara wa NMB, Filbert Mponzi
akishirikiana na Mkuu wa idara ya Bima wa NMB, Martin Massawe ikilenga
kuongeza uelewa wa huduma za bima nchi kote sambamba na kupata Wateja
wapya wa huduma hiyo.
Afisa Mkuu kitengo cha Wateja binafsi wa
NMB, Filbert Mponzi alisema licha ya elimu juu ya bima kuongezeka, bado
kuna watanzania wengi hawatumii huduma hizi. Takwimu zinaonesha ni
asilimia 15 tu ya watanzania wanaotumia huduma mbalimbali za Bima.
Benki
ya NMB inazo huduma tofauti za Bima inazoshirikiana na kampuni tofauti
za Bima ambazo zinapatikana kwenye matawi 226 ya NMB nchini kote,
mtandaoni kupitia Mkononi plus Kwa piga *150*68# au popote pale ulipo
mpaka mahali ambako kampuni za Bima hazijafika.
Bima zinatolewa na Benki ya NMB ni Bima ya ujenzi, Afya, kilimo, Chombo cha moto, maisha, Mali n.k
Benki
ya NMB imeshirikiana na kampuni zinazoaminika nchini ambazo ni Sanlam
Life, Shirima la Bima la Taifa(NIC), Jubilee insurance, Jubilee life,
Metropolitan life, Britain Insurance na shirima la Bima Zanzibar(ZIC)
hivyo inauhakika ya kukidhi mahitaji yote ya wateja.
Tuesday, March 8, 2022

BENKI YA NMB YAZINDUA MSIMU WA PILI 'UMEBIMA' KWA KISHINDO JIJINI DAR LEO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment