Ofisa Mfawidhi wa TASAC Mkoa wa Tanga Captain Christopher Shalua akizungumza wakati wa ziara hiyo |
MWENYEKITI
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC)
Captain Mussa Mandia kushoto akimsikiliza Mwenyekiti wa Kijiji cha
Kipumbwi wakati wa ziara yake |
NA OSCAR ASSENGA, PANGANI
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli
Tanzania (TASAC) Captain Mussa Mandia ametoa wito kwa wavuvi na
wasafirishaji Kata ya Kipumbwi wilayani Pangani Mkoani Tanga kuacha
kutumia vyombo vya kubebea mizigo kwa ajili ya kusafiria badala yake
watumie vile vilivyoruhusiwa kisheria.
Hatua hiyo inatokana na
eneo la Kipumbwi kushamiri vitendo vya abiria na mizigo kupanda kwenye
vyombo vya kusafirishia mizigo kufanya safari zao kati ya Kipumbwi
kuelekea Visiwa vya Unguja na Pemba na hivyo kuhatarisha usalama wa
maisha yao na mali.
Captain Mandia aliyasema hayo wakati wa
ziara kuitambulisha bodi ya Wakurugenzi ya Shirika hilo ambao wapo
mkoani Tanga ambapo walianzia kwa kutembelea Bandari ya Tanga na maeneo
mengine lengo ni kusikia changamoto walizonazo kwenye eneo la kipumbwi
na kuona namna ya kuzifanyia kazi
Alisema kwao Kama Shirika
wanasimamia ulinzi na usalama wa usafiri majini hivyo Serikali itachukua
njia nzuri za usafiri bila kupoteza maisha na mali zenu hivyo alihaidia
kulichukua suala hilo na kuhakikisha linafanyiwa kazi.
“Sisi
kama Shirika jukumu letu ni kusimamia ulinzi na usalama niwahaidi suala
la chombo cha usafiri hapa Kipumbwi tunalichukua na kuona namna
linafanyiwa kazi”Alisema
“Hata leo asubuhi wakati nazungumza na
Mkuu wa wilaya ya Pangani nimemueleza tutakachofanya kwa mamlaka
tulionayo ni kuangalia namna ya kuboresha sheria, kanuni na taratibu
tulizonazo kufikia mahali ambapo kutakuwa na vyombo vizuri kwa ajili ya
kusafisha watu”Alisema Captain Mandia
Hata hivyo aliwaambie
wananchi wa eneo hilo kwamba chao kimefika serikali na watalifanyia kazi
ili kuona namna ya kulipatia ufumbuzi kwa lengo la kuondosha changamoto
iliyopo.
Akizungumzia suala la Light House kwenye eneo
hilo,Captain Mandia alisema kwamba wao Shirika wanajukumu la kudhibiti
vyombo vya usafiri hivyo watawaelekeza Bandari kwamba kila
wanaporasimisha wajitahidi kuhakikisha kuweka vitu ambavyo vinahitajika
ili kuwasaidia wananchi ikiwemo kuweka (Light Huose) Taa,
Alisema
taa hizo ambazo zitakuwa zikiwaka zitakuwa zikiashiria eneo husika ili
kuweza kuwaepusha kupotea wanapokuwa majini wakiendelea na shughuli za
uvuvi.
Kuhusu chombo cha uokoaji alisema tayari wao Tasac
wanakuja na utaratibu huo na inategemea na bajeti maana nchi inasehemu
kubwa sana ya maji hivyo wamelichukua na kuona namna ya kulifanyia kazi.
“Lakini kitu ambacho mngeweza kukifanya wavuvi na
wasafirishaji mizigo wapeni elimu lugha ya kuwasiliana bahati nzuri wana
simu za mikononi zinatumia satelite kwa hiyo wachukue kuna frequare
ambazo wanatumia namba za simu wanazotumia kwa hapa wawasiliane na
Bandari ya Tanga na Pengine Pangani ni rahisi mtu kusema tupo eneo
Fulani tunahitaji msaada ili kuweza kuwasaidia kuwaokoa wanapopata
majanga baharini”Alisema Captain Mandia.
No comments:
Post a Comment