TotalEnergies TANZANIA YASHEREKEA SIKU YA WAPENDANAO KWA KUTOA ZAWADI KWA WATEJA WAO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 14, 2022

TotalEnergies TANZANIA YASHEREKEA SIKU YA WAPENDANAO KWA KUTOA ZAWADI KWA WATEJA WAO


Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Mawasiliano wa kampuni ya TotalEnergies Getrude Mpangile akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wapendanao na kueleza kuwa kampuni hiyo itaendelea kuwa kinara katika utoaji wa huduma za mafuta, vilainishi na huduma zisizo za mafuta hafla iliyofanyika leo katika kituo cha mafuta cha TotalEnergies Samora jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Huduma zisizo za mafuta zinazotolewa katika maduka ya Bonjour Jane Mwita akizungumza na waandishi wa habari wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wapendanao na kueleza kuwa kampeni hiyo itaendelea hadi Februari 27, mwaka huu.

Kampuni ya Mafuta ya TotalEnergies imeadhimisha Siku ya Wapendanao 'Valentine's' kwa kutoa zawadi mbalimbali kwa wateja wao wanaopata huduma katika vituo vyao  ikiwemo huduma za kujaza mafuta, kubadili oili, kupata huduma katika maduka ya Bonjour na kuosha magari.

Akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyofanyika katika kituo cha mafuta cha Samora jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Mawasiliano Getrude Mpangile amesema kuwa katika maadhimisho ya msimu huu wa Siku ya Wapendanao kampuni ya TotalEnergies itaendelea kutoa zawadi kwa wateja wao kama sehemu ya kusherekea maadhimisho hayo.

Amesema kuwa kampuni hiyo ya mafuta namba moja nchini imekuwa ikitoa huduma bora na salama kwa vifaa vya usafiri ikiwemo mafuta  yanayotunza  injini pamoja na huduma nyingine ikiwemo kubadilisha oili, kuosha magari  pamoja na kupata bidhaa mbalimbali kwenye maduka ya Bonjour.

Kwa upande wake Meneja wa Huduma zisizo za mafuta zinazotolewa katika maduka ya Bonjour Jane Mwita amesema mteja akinunua chokoleti 2 za Cadbury Dairy Milk katika maduka ya Bonjour yaliyopo katika vituo vya mafuta Samora, Uhuru na University jijini Dar es Salaam anapata Chokoleti moja ya Cadbury P.S bure zikiwa na ujumbe maalumu katika msimu huu wa Valentine's na wateja watakaotembelea vituo katika siku ya wapendanao wakiwa wamevalia nguo nyekundu watapatiwa zawadi mbalimbali.

Amesema promosheni hiyo itaendelea hadi Februari 27 katika vituo vya TotalEnergies Samora, Uhuru na University jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Mawasiliano Getrude Mpangile akigawa zawadi kwa wateja waliotembelea na kupata huduma katika kituo cha mafuta cha TotalEnergies Samora jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad